Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir.
Wafungwa
walioachiwa ni pamoja na Pagan Amum, katibu mkuu wa zamani wa chama tawala cha
Sudan People’s Liberation Movement (SPLM), Majak D’Agot, Oyai Deng Ajak na
Ezekiel Lol Gatkuot
Serikali ya Sudan Kusini inatarajia kufikia hatua za
kimaendeleo katika mashauriano ya amani na waasi, kufuatia kuachiwa kwa
wafungwa wa kisiasa walioshukiwa kupanga njama za kuiangusha serikali ya Rais
Salva Kiir, kwa mujibu wa msemaji wa Rais, Ateny Wek Ateny.
Duru ijayo ya
mazungumzo ya nchi za jumuiya ya IGAD inayofadhili mazungumzo ya amani
yanayofanyika katika nchi jirani ya Ethiopia imepangwa kuanza leo Jumatatu
katika mji mkuu Addis Ababa.
Wafungwa
walioachiwa ni pamoja na Pagan Amum, katibu mkuu wa zamani wa chama tawala cha
Sudan People’s Liberation Movement (SPLM), Majak D’Agot, Oyai Deng Ajak na
Ezekiel Lol Gatkuoth.
Kuachiwa kwa
wafungwa hao kumekuwa moja ya dai kubwa kutoka kwa wawakilishi wa waasi waliopo
kwenye mashauriano ya amani, ambao wanamuunga mkono makamu rais wa zamani
Riek Machar.
CHANZO VOA SWAHILI
No comments:
Post a Comment