Kabichi
Wengi tumekuwa na mawazo mgando kuwa
kabichi inafaa kwa kupikwa kama mboga na kuishia hapo.
Wapo pia wanaofahamu kuwa kabichi ni
maalumu kwa ajili ya kutengeneza Salad au kachumbari inayotumika kuongeza ladha
kwenye mlo.
Lakini ukweli ni kwamba kabichi ina
manufaa mengi mno kiafya hasa kwa mtu anayekula mboga hii ikiwa imetayarishwa
kwa kuzingatia kanuni zote za kiafya.
Vitamin K inayopatikana katika majani
haya hufanya kazi kama chakula cha ubongo, kabichi husaidia kwa kiasi kikubwa
mlaji kuwa na uwezo mzuri wa kufikiri.
Kwa mujibu wa jarida la Health Living
kabichi ina uwezo wa kuzuia na kukabiliana na magojwa mbalimbali nyemelezi kwa
ubongo.
Vilevile kabichi inatajwa kupunguza
makali ya ugonjwa wa saratani ya matiti kwa wanawake. Inaelezwa kuwa tishu
zilizopo ndani ya mboga hii huzuia kukua kasi ya ugonjwa wa saratani ya matiti.
Kwa wenye tatizo la kuumwa kichwa mara
kwa mara supu inayotokana na kabichi iliyochemshwa ni dawa inayoweza
kukabiliana na hali hiyo ndani ya muda mfupi. Kwa wale wenye ngozi yenye mafuta
na kushambuliwa na chunusi sugu kabichi ina uwezo wa kukausha mafuta na kuiacha
ngozi ikiwa kwenye hali ya ukavu.
Kabichi pia inatajwa kuwa kichocheo
katika mzunguko wa damu na kuifanya itiririke na kuzunguka vizuri katika
mishipa ya damu.
CHANZO, MWANANCHI
No comments:
Post a Comment