Na Mwandishi Wetu.
MAZOEZI ya warembo watakaowania taji la urembo la Sinza, Miss 2014 yataanza Mei 5 kwenye ukumbi wa Meeda uliopo Sinza Mori na Lufungila jijini.
Taji la Miss Sinza linashikiliwa na Miss Tanzania, Prisca Clement alimaliza katika hatua ya 10 bora katika mashindano ya mwaka jana ya Miss Tanzania na pia alishinda taji la mrembo mwenye kipaji katika mashindano hayo.
Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema kuwa maandalizi ya mazoezi hayo yamekamilika na yatasimiwa na kamati ya maandalizi huku ikitafuta mwalimu kwa ajili ya kuwanoa.
Majuto alisema kuwa warembo waliowahi kushiriki mashindano hayo wanaruhusiwa kuja kutoa sapoti kwa warembo wapya na kamati yao itawapa nafasi ya kuwafundisha warembo wapya ili kuwapa ‘mbinu’ mbali mbali za mashindano hayo.
Alisema kuwa fomu za kuomba kushiriki katika mashindano hayo zinapatikana kuanzia leo (Ijumaa) maduka ya Zizzou, Sinza Afrika Sana, Meeda, Ofisi za Miss Tanzania na Ofisi za gazeti la Mwananchi (Tabata reline.
“ Lengo letu kubwa ni kurudisha hadhi ya Miss Sinza, Kinondoni katika mashindano ya mwaka huu, tumejipanga kulinda heshima yetu na tunaamini titafanikiwa kwa heshima ya wakazi wa Sinza, Kinondoni na Tanzania kwa ujumla,” alisema Majuto.
Alisema kuwa wanawakaribisha warembo wanaotaka ‘kupata taji’ kuchukua fomu zao ambazo zinatolewa bure. Majuto pia aliwaomba wadhamini wanaotaka kujitangaza kupitia mashindano yao wanaruhusiwa kuja kudhamini mashindano hayo na milango ipo wazi.
CHANZO, MPENJABLOG
No comments:
Post a Comment