Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 30 April 2014

SHULE YATENGA SHS. 90 MILIONI KWA WANAFUNZI WANAOTOKA MAZINGIRA MAGUMU


Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot.com, Arusha

SHULE ya Sekondari Edmund iliopo Sinon Mjini Arusha imetenga zaidi Shs. 90 milioni kwa wanafunzi 90 kila mwaka kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaotokea katika mazingira magumu huku lengo likiwa ni kuwaepusha na mimba za utotoni lakini pia uvunjifu wa amani kwenye jamii.
Fedha hizo zinatolewa na wafadhili wa nje ya nchi pamoja na mfuko wa shule hiyo ujulikanao kama Mfuko wa Edmund ambao pia huo unalenga kuhamasisha ufadhili wa ndani.
Hayo yameelezwa na Mkwabi Francis ambaye ni mkuu wa shule hiyo wakati akiongea na wanafunzi, wazazi pamoja na walezi wa shule hiyo kwenye maafali ya nane ambapo jumla ya wanafunzi 240 wanatarajia kuhitimu katika shule hiyo.
Mkwabi alisema kuwa mpango huo wa kuwasidia watoto wanaotokea katika mazingira magumu umeweza kuwanufaisha watoto wanaotokea katika vijiji vya Murieth, Mkono,Nadosoito,Unga Limited, na Sinoni ambapo walengwa ni wale wenye maitaji muhimu.
Alifafanua kuwa walengwa hao ni wale watoto wanaotokea katika familia ambazo hazina uwezo,na mayatima ambapo watoto hao huweza kukupewa ufadhili maalumu kwa ajili ya kusoma na kupata elimu ya Sekondari.
"Wafadhili wetu wakubwa wanatokea katika Nchi za Ausralia, Newzeland,Iland, na Marekani na hawa wanatufanikikishia hawa watoto 90 kuweza kupata elimu yao bora sana ya Sekondari ingawaje na sasa sisi tumejipanga kuhakikisha kuwa na sisi hapa hapa shuleni tunatoa ufadhili kwa watoto wetu ili siku hata kama tukikosa wafadhili basi tunaweza kusaidia jamii'aliongeza Mkwabi.
Pia alisema kuwa nao wazazi wanapaswa kujua na kutambua kuwa nao wana nafasi kubwa sana ya kuweza kuwasaidia watoto hasa wale ambao hawana uwezo wa kupata elimu ya sekondari kwani kupitia njia ya ufadhili wa ndani inawezekana kabisa 
"Kama wazazi, na walezi wakiwa na tabia ya kuchangia sekta ya maendeleo ya shule hasa mifuko ya shule  basi wataweza kusaidia jamii na hatutaweza kuwategemea zaidi wafadhili ambao wanatokea nje ya nchi kwani wakati mwingine wanapokatisha ufadhili wao wanasababisha watoto wawe kwenye hali ya uoga," aliongeza Mkwabi.
Wakati huo huo Wanafunzi wa shule hiyo ambao ni wahitimu waliwashauri walimu wa shule hiyo lakini pia wale wa shule nyingine kuachana na tabia ya kuwatenganisha wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka cha nne dhidi ya wale wa kidato cha tano na sita kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha wale wa vidato vya chini kutopata hamasa ya kujiunga au kufanya vema ili kuweza kujiunga na kidato cha tano na sita.

No comments:

Post a Comment