Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 29 April 2014

MAMA SHUJAA WA CHAKULA WAINGIA RASMI KIJIJI CHA MAISHA PLUS, PROFESA ANNA TIBAIJUKA MGENI RASMI KATIKA SHEREHE HIZO.


Profesa 
Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi wa pili 
kutoka kulia pamoja na Babu wa Kijiji cha Maisha Plus akiwasalimia
akina mama Shujaa wa Chakula ambao wameingia Rasmi Kijiji cha Maisha 
Plus Jana usiku.


Akina 
Mama Shujaa wa Chakula Wakiwa wanamuimbia wimbo maalum Profesa Anna 
Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi mara baada ya 
kuwasili Kijijini hapo.


Hawa ndio Mama Shujaa wa Chakula ambao jana usiku wameingia Rasmi katika Kijiji Cha Maisha Plus


Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhudia Kukaribishwa Rasmi kwa Mama shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus.

Mshindiwa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012 Sister Anna Mwasu wa tatukutoka kulia akiwa katika sherehe za kuwakaribisha mama Shujaa waChakula ambao  wameingia rasmi katika Kijiji cha Maisha Plus Jana.


Mwakilishi  
kutoka Forum CC Faidhari akizungumza jambo wakati wa kuwakaribisha Mama 
Shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus.


Teresa Yates Mwakilishi kutoka OXFAM akitoa salama za Shukurani kwa wadau wote


Mkuu 
wa Wilaya ya Bagamoyo Mh. Ahmed Kipozi akiwakaribisha Rasmi
wageni wote katika Kijiji cha Maisha plus pia kumkaribisha Mgeni Rasmi
Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi
ili aweze kutoa hotuba yake.


Profesa
Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi wa
katikati akitoa hotuba yake fupi wakati wa Sherehe za kuwakaribisha Mama 
Shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus, katika Hotuba hiyo
aliwapongeza waandaaji na wabunifu wa Shindano hilo, pia Grow kupitia
OXFAM kwa kuungana na Maisha Plus kuwaleta Mama Shujaa wa Chakula,
Mwisho aliahidi kuongeza Milioni 5 kwa Mama Shujaa wa Chakula atakaye
nyakua ushindi, Kutoa Milioni mbili na nusu kwa Mama Shujaa wa Chakula
aliyepita ili zikamsaidie katika kilimo na Mwisho Kutoa Milioni Mbili
kwa Washiriki wa Shindano la Maisha Plus ambao sasa wamebakia 16 mpaka 
mwisho wa Shindano Tarehe 18.05.2014


Mmoja 
wa washiriki wa Maisha Plus akisoma Jina la Mama yake ambaye atakuwa 
naye katika Kipindi hiki kilicho bakia cha Shindano la Maisha Plus/ Mama 
Shujaa wa Chakula.
 

Vijana na Washiriki wa Maisha Plus wakiwa na Mama zao walezi ambao ndio wameingia Rasmi kijijini Jana


Huyu Ndiye Mama Shujaa wa Kwanza kupata nafasi ya Kuwa Markia wa Kijiji cha Maisha Plus Mary J. Mwanga, na wa kwanza kulia ni Rais wa Kijiji cha Maisha Plus Abisai Caron kutoka kenya hapa akiwa anavishwa kofia ya utambulisho na Epheta Msiga Meneja Miradi kutoka DMB


Picha ya Pamoja Mgeni Rasmi  Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi, Wakina Mama Shujaa wa Chakula, Vijana wa Maisha Plus pamoja na wadau mbalimbali waliofika katika sherehe za kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula  Kijiji cha maisha Plus

Mkurugenzi Mtendaji wa DMB ambao ndio waendeshaji wa Shindano la Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula Ally Masoud(Masoud Kipanya) Akitoa utaratibu wa jinsi Akina mama Shujaa wa Chakula watakavyo ishi na vijana hao katika kijiji hicho


Mama  Shujaa wa Chakula wakipata maelekezo Mbalimbali juu ya Kijiji Hicho

 
Moja 
ya Bendi Matata kutoka Bagamoyo wakiwa wanatumbuiza nyimbo Nzuri wakati 
wa kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji Cha maisha Plus


Wakipokea maelekezo kadha wa kadha
MAISHA PLUS/ MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2014

CHANZO,FULL SHANGWE 

No comments:

Post a Comment