Irenei Kiria
Tunapenda kuipongeza serikali na hasa kumpongeza kwa
dhati Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kukubali kuanziha mchakato wa
kutunga katiba mya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tunalishukuru
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutunga sheria zote
zinazowezesha kuelekeza hatua mbali mbali za mchakato huu.
Tunaishukuru
Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Uongozi wa Jaji Joseph Sinde
Warioba kwa kuendesha zoezi la kukusanya maoni kutoka kwa wananchi na
kuandika rasimu ya kwanza nay a pili za Katiba Mpya.
Tunawashukuru
wananchi, wataalamu na Asasi mbali mbali kwa kushiriki na kutoa maoni
katika hatua mbali mbali za mchakato huu wa kutunga Katia Mpya.
Kutokana na namna mambo yananvyokwenda katika Bunge Maalum la kutunga Katiba, Asasi za Kiraia ziliona umuhimu
kukutana kuanzisha tarehe 8 Aprili 2014 kutafakari yanayojiri na
kukubaliana utakuwa mchango wa Asasi katika kuhakikisha Tanzania inapata
katiba mpya inayokidhi mahitaji ya sasa na ya vizazi vijavyo. Baada ya
vikao vya mara kwa mara na majadiliano mengi pamoja na kukusanya taarifa
kadhaa. Hatimaye katka kikao cha tarehe 15 Aprili 2014 tulikubaliana
tamko.
Kwa hiyo sisi Asasi za Kiraia tumekubaliana ya kwamba:
Kwa
kuwa huu ndiyo mchakato pekee hapa Tanzania wa kutunga katiba mpya
ambao umewahusisha wananchi tangu hatua za awali, tunauunga mkono na
kuutakia mafanikio.
Kwa kuwa Rais wa Jamhuri wa Tanzania
amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha katiba mpya inapatikana kabla ya
kipidi chake cha uongozi kuisha, ni vema Bunge Maalum la Katiba
likazingatia yafuatayo;
1. Sisi Asasi za Kiraia
tunaunga mkono Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya kama ilivyowasilishwa na
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, kwa kuwa imekidhi mahitaji ya Watanzania
wa sasa na vizazi vijavyo kama ikipita itaimarisha uadilifu, uwazi,
uwajibikaji, amani na umoja wetu.
2. Kwamba
hatujafurahishwa na mijadala ndani ya Bunge Maalum la Kutunga Katiba
mijadala ambayo imepoteza utaifa na badala yake imejikita kwenye
kutoheshimiana, ubabe, ubaguzi, vijembe na vitisho.
3.
Kwamba tumehuzunishwa sana na tabia ya kudhihakiana na kudharau Rasimy
ya pili ya Katiba pmoja na tume ya mabadiliko ya katiba na hasa
Mwenyekiti wake.
4. Tunaona kwamba mwennendo wa
mijadala ni kuelekea kutetea maslahi ya watawala wa vyama vya siasa
badala ya maslahi ya utaifa na ustawi wa wananchi.
5.
Kwamba kitendo cha baadhi ya wajumbe kupendekeza kutoa maneno;
uwajibikaji, uadilifu, uwazi katika kipengele cha tunu za taifa inatia
mashaka kama nia ya Bunge Maalum la Katiba ni kutuletea katiba
itakayotutatulia matatizo hayo.
6. Kwamba
hatufurahishwi na malumbano yasiyo na tija yanayochukua muda mrefu
kwenye mambo madogo madogo. Hii inapelekea kupoteza muda na hivyo
kutumia rasilimali za umma vibaya.
7. Kwamba
hatujafurahishwa na kufungwa kwa tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Na pia hakuna juhudi za serikali kuwafikishia wananchi Rasimu ya Katiba
mpya na kuwaelimisha maudhui yake.
8.
Tumeelewana kwamba tulikosea kutuga sheria inayohusu wabunge wa
kuchaguliwa kushiriki katika bunge maalum la katiba. Kwa kawaida
watatetea maslahi yao kwanza kabla ya maslahi ya wananchi. Mfano bunge
la Tanzania lina wabunge 357, lakini rasimu inapendekeza wabunge 75 tu.
Hili ni tishio la wazi kwa maisha ya kisiasa ya baadae ya wabunge
madalakani sasa na hivyo wanapata umoja wa kupambana kuhakikisha rasimu
hii isipate ka ilivyo.
9. Tunaelewa pia kwamba,
Rasimu hii imependekezwa kupunguza madaraka ya Rais ya kuteua viongozi
na watendaji wa serikali. Jambo hili, kwa mtazamo wetu ni tishio kwa
wagombea urais kwamba hawatakuwa na nguvu ya kuahidi wapambe wao nafasi
za uteuzi ili wawaunge mkono kwenye kampeni ya uchaguzi.
Rai yetu Umoja wa AZAKI.
Tunasihi wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Uongozi wa Bunge hilo kurekebisha hizo kasoro walizozieleza.
Irenei Kiria
Mwenyekiti wa Umoja wa Asasi za Kiraia (AZAKI).
No comments:
Post a Comment