Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday, 28 April 2014

VITAMBULISHO VYA BIMA NI LULU- NHIF

DSC07977
Afisa wa Mfuko wa Taifa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Singida, Isaya Shekifu akiwahamasisha madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Singida, juu ya umuhimu wa kujiunga na mfuko huo ili kujihakikishia kupata matibabu hata wakati hawana fedha.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
WANACHAMA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Singida wameaswa kutunza vizuri vitambulisho vyao kwa madai kuwa vitambulisho hivyo ni sawa na kuwa na fedha taslimu.
Afisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Singida,Isaya Shekifu ametoa wito huo hivi karibuni wakati akihamasisha na kuwaelimisha madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Singida, juu ya umuhimu wa kujiunga na mfuko huo ili wawe na uhakika kupata matibabu wakati wote hata kama hawana fedha.
Akifafanua, amesema kila mwanachama wa NHIF, anao wajibu wa kuhakikisha anakitunza vizuri kitambulisho chake ambacho  ni sawa na fedha pia ni sawa na daktari na dawa.
“Kitambulisho cha NHIF chenyewe kinakuhakikishia kupata matibabu,kumwona daktari na kupatiwa vipimo na dawa bila kuongeza malipo mengine zaidi ya malipo ya uanachama wa mfuko huo.
“Kutokana na ukweli huo basi vitambulisho hivi vina thamani kubwa hivyo vinapaswa kutunzwa vizuri sawa sawa na unavyotunza fedha zako”,alifafanua zaidi Shekifu.
Afisa huyo alitaja wajibu mwingine wa mwanachama wa mfuko huo kuwa ni kurejesha vitambulisho pindi uanachama unapokoma na kuheshimu taratibu za rufaa na taaluma za uganga na uuguzi na tiba kwa ujumla.
Katika hatua nyingine,Shekifu amesema mwanachama akipoteza kitambulisho atapatiwa kitambulisho kingine baada ya mwezi moja.
“Ada ya kubadili kitambulisho kwa sababu ya kupotea kwa mara ya kwanza atatozwa shilingi 20,000 na shilingi 50,000 akipoteza kwa mara ya pili na kuendelea Hayo ni mabadiliko ya hivi karibuni”,amesema.
Aidha, Shekifu alitaja baadhi ya mafao yanayotolewa na mfuko huo kwa wananchama wake ni pamoja na kulazwa wodi gredi ya kwanza na ya pili,upasuaji kuanzia mdogo,mkubwa na unaofanywa na madaktari bingwa,miwani ya kusomea na kuonea na matibabu kwa wastaafu.
Kwa mujibu wa Shekifu,mkoa wa Singida unao vituo 205 vya kutolea huduma ya matibabu kwa wananchama wa NHIF.
CHANZO, MOBLOG

No comments:

Post a Comment