Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 30 April 2014

WANACHAMA 1,000 UVCCM MERU WAFUNGA BARABARA ARUSHA


Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida vijana zaidi ya 1000 ambao ni wanachama wa umoja wa vijana chama cha mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Meru mkoa wa Arusha wamevamia ofisi za chama hicho kuanzia ngazi ya Wilaya hadi mkoa huku wakidai kuwa Makao makuu ya chama hicho wamewaonea kwa kutangaza uamuzi wao wa kuwachagulia viongozi tofauti na matakwa yao ambapo wao walimchagua Kamanda wao ambaye Ni John Palangyo ila CCM makao makuu walitofautiana nao.
hataivyo maandamano hayo ambayo yaliratibiwa na wajumbe wa UVCCM Meru yaliweza kusababisha shuguli mbalimbali za chama hicho kuanzia ofisi ya Wilaya hadi Mkoa kusimama kwa kuwa wajumbe hao walilazimika kuingia kwa nguvu ndani ya ofisi hizo na kisha kushinikiza kusikilizwa kwa madai yao
Akiongea kwa niaba ya wajumbe hao mmoja wa wajumbe hao Joshua Mbwana "Mwarabu"alisema kuwa kilichosababisha waweze kufanya maandamano hayo ambayo yalianzia kuanzia eneo la Usa River Mpaka Arusha ni kuelezea umma kuwa wapo baadhi ya viongozi katika chama hicho ambao wanawachagulia viongozi wa kuwaongoza bila kuwauliza
"hivi juzi tulikuwa na tulimchagua kamanda wetu ambaye ni John Palangyo na tulimpitisha lakini baada ya jina kufika mkoani ghafa jina lilibadilishwa kama haitoshi makao makuu wakasema kuwa wana mtu wao sasa je wao ndio wanatuchagulia mtu wa kutuongoza au sisi kamwe hatutakubali na badala yake tutapigana hadi mwisho hii tabia imetucosha sana"aliongeza Joshua

wakati huo huo alidai kuwa endapo kama hali hiyo itaendelea kufanyika ambapo wananchi, wajumbe, na wanachama watachagua kiongozi alafu makao makuu pamoja na uongozi wa Mkoa wakakataa basi mapambano yatakuwa makubwa sana.
Kutokana na hilo mjumbe huyo alisema kuwa pamoja na kuwa wamevamia ofisi za CCM wakiwa wanachama zaidi ya 300 bado kama hawatapewa majibu yha kuridhisha juu ya kamanda wa vijana ambaye amechaguliwa kwa kura zote na wajumbe wa baraza hilo basi ndani ya siku nne kutoka sasa huenda wakaandamana hadi makao makuu ya ofisi za CCM
"Tumesharatibu maandamano hayo na yataenda vizuri itakuwa ni histori a kwa CCM kuchagulia viongozi kwa maslahi yao binafsi na matakwa ya viongozi wa ngazi za juu hasa wale ambao wana malengo ya kugombea nafasi za ubunge katika majimbo kwani ujumbe wetu ni lazima tutauweka wazi na kila mtu aweze kuosoma lakini hata kuingia ndani ya ofisi hizo bila taarifa wala kibali cha aina yoyote ile"aliongeza Joshua.
Hata hivyo, Katibu wa chama hicho Wilaya ya Meru, Langaeli Akyoo alisema kuwa mchakato wa kumpata kiongozi ambaye vijana hao wanamtaka ulienda vizuri na majina matatu yalifikishwa Dar es saalam makao makuu lakini baadaye hayakurudi kama ilivyoratarjiwa
Akyoo alisema kuwa majina mawili yalirudi majina mawili ambayo yana utata mkubwa ambapo utata huo ndio uliosababisha maandamano makubwa kuanzia Meru hadi Arusha.
"Jamani maombi yenu nimeyapata na ninapenda kuwaambia kuwa majina ambayo yalienda Dar es saalam makao makuu yalirudishwa mawili ambayo yana utata na wao walisema kuwa mchakato unatakiwa kuanza moja jambo ambalo sisi hatukubalini nalo kabisa"aliongeza Akyoo
Awali mwenyekiti wa umoja wa vijana Wilaya hiyo Bw Elirehema Mbisse alisema kuwa mchakato wa kumpata Kamanda huyo unaendelea na hivyo amewataka wawe na subira ili waweze kuangalia namna ya kutatua tatizo hilo ambalo limesababisha ofisi za CCM  kusimamisha kazi kwa muda.
Uongozi wa Uvccm kupitia kikao chake cha kamati ya utekelezaji kilipendekeza majina matatu ambayo ni John .D. Palangyo, Sioi Solomoni Sumari, na Daniel Mirisho Palangyo,na baadaye muhtasari uliweza kupelekwa mkoani ambapo Mkoa ulijiridhisha na majina hayo na uliweza kuhoji na hatimaye waliweza kumpata John.D. Palangyo kama Kamanda wa Vijana Wilaya ya Meru, lakini baadaye barua ilikuja na kudai kuwa kamanda wa Meru siyo huyo jambo ambalo si la kweli.

No comments:

Post a Comment