Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 30 April 2014

SERIKALI YASHAURIWA KUANGALIA SHULE YA ILBORU


Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha

SERIKALI imeombwa kuendelea kutenga fedha za ukarabati wa majengo kila mwaka kwa shule Ilboru iliyopo jijini Arusha ili kujenga mazingira mazuri mazuri ya kujifunzia na kufundishia yatakayofanya shule hiyo iweze kuonekana kama shule ya kipaji maalumu kwani majengo ya sasa yalijengwa toka mwaka 1946.
Hayo yalisemwa na mkuu wa shule ya sekondari hiyo Julius Shula alipokuwa akizungumza na wadau na wazazi katika mahafali ya 21 ya kidato cha sita yaliyofanyika shuleni hapo ambapo jumla ya wahitimu 153 walitnukiwa vyeti vyao.
Shula alisema kuwa serikali inapaswa kuendelea kutenga fedha za ukarabati kila mwaka haswa kwa shule kongwe zenye wanafunzi wenye vipaji maalum kiakili ili walau iweze kuwafanya wanafunzi hao kujituma zaidi kwa kuwa kuwepo kwa mazingira mazuri ya kujifnzia kunachangia hata wanafunzi kfanya vizuri katika masomo yao.
Alieleza kuwa shule hiyo imepata mafanikio makubwa katika eneo la ukarabati wa baadhi ya  majengo na miundombinu mingine baada ya serikali kutoa kiasi cha shilingi milioni 100 ambapo kupitia fedha hizo waliweza kukarabati mabweni sita pamoja na bwalo ambapo ukarabati huo umechangia sana kuongeza kiwango cha ufaulu shuleni hapo.
“Naishauri serikali yetu sikivu iendelee kutenga fedha za ukarabati wa majengo kwa kila mwaka ili kuzijengea mazingira ya kujifunzia na kufundishia hali hii itachangia sana kuwafanya wanafuzi wajitume zaidi katika kufanya vizuri katika masomo yao,” aliongeza Shula.
Alidai kuwa pamoja na shule hiyo kuwa na mafanikio ya kitaaluma lakini bado inakabiliwa na changamoto ya upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi hali inayosababisha shule kutafuta walimu wa muda ambao malipo yao ni makubwa sana kwa mwezi huku shule ikiwa haina uwezo wa kumudu gharama hizo.
Alitaja changamoto ingine kuwa ni pamoja na uchakavu mkubwa wa madarasa pamoja na nyumba za watumishi ambapo wanafunzi wanakosa mahali pazuri pa kujifunzia kutokana na uchakavu mkubwa wa madarasa huku nazo nyumba za walimu zikiwa zinakatisha tama kwa kuwa nyumba wanazoishi sio rafiki kabisa.

No comments:

Post a Comment