Hali ya
taharuki imetanda mjini Bangui kutokana na vita vya wenyewe ka wenyewe
Walinda
amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, wamewasindikiza zaidi ya
waisilamu,1,200, kutoka katika mji mkuu wa CAR Bangui kutokana na tisho kwa
usalama wao.
Waisilamu
hao ni baadhi ya waisilamu waliosalia mjini Bangui ambao walilengwa
kushambuliwa na wakristo katika mzozo wa wenyewe kwa wenyewe.
Nchi
hiyo imekuwa ikikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu waasi wa Seleka,
kupindua serikali mwezi Machi mwaka jana.
Waasi
hao wa Seleka walituhumiwa kwa kuwashambulia wakristo na kuchochea ghasia hizo
zaidi. Gasia zilizozuka hata hivyo zilikuwa za kulipiza kisasi.
Pia
kulikuwa na ripoti kwamba watu 22 wakiwemo machifu 15 na wafanyakazi wa shirika
la Medecins Sans Frontieres (MSF), waliuawa mjini Nanga Boguila.
Mauaji
hayo yalifanyika siku ya Jumamosi wengi wa waathiri wa wakiuawa wakati kliniki
ya shirika hilo iliposhambuliwa.
Punde
tu msafara huo ulipoondoka mjini Bangui, watu walivamia nyumba na majumba ya
biashara yaliyokuwa yanamilikiwa na waisilamu hao na hata pia kuvamia msikiti.
"hatukuwataka
waisilamu hapa na wala hatutaki msikiti wao,'' alisema mvamizi mmoja kwa jina
Guy.
Waisilamu
wachache sana wamebaki mjini Bangui lakini maelfu wametoroka katika siku za
hivi karibuni, huku hali ya taharuki ikiendelea kutanda.
Shirika
la Amnesty International limetuhumu walinda amani kwa kukosa kuzuia mauaji ya
halaiki.
No comments:
Post a Comment