Je unamkumbuka kijana aliyejificha katika
gurudumu la ndege na kusafiri kutoka Carlifonia hadi Hawaii nchini Marekani?
Mamake
kijana huyo aliyenusurika kifo wakati wa safari yake ya saa tano angani ,
amepigwa na mshangao kujua kuwa kijana wake yuko hai na kuwa alipanda ndege
hiyo akidhani ilikuwa inaeleklea Somalia, ili aweze kurejea nyumbani.
Mama huyo, Ubah Mohamed
Abdullahi, anayeishi katika kambi ya wakimbizi nchini Ethiopia, anasema kuwa
ilikuwa mara yake ya kwanza kusikia kuhusu kijana wake ambaye alipotea miaka
sita iliyopita.
Mama
Uba ambaye alitalakiana na mumewe, alisema hakuwahi kuwasiliana na familia yake
yake iliyohamia nchini Marekani mwaka 2008.
Babake
kijana huyo menye umri wa miaka 16 alisema kuwa alikuwa anajaribu kurejea
Somalia na kwamba alidhani ndege hiyo ilikuwa inaelekea Somalia ili aweze
kwenda kumuona mamake.
Yahya
Abdi alisafiri bila ya hewa ya Oksijeni akiwa angani kwenye baridi kali kwa saa
tano kutoka Carlifonia hadi Hawaii.
Mama
Abdullahi alisema kuwa alipokea taarifa kutoka kwa jamaa wake wanaoishi Ulaya
kuhusu mtoto wake na alivyonusurika kifo.
Akiongea
na BBC kutoka katika kambi ya wakimbizi ya Sheed Dheer ambako amekuwa akiishi
tangu mwaka 2008,mama huyo Abdullahi alisema kuwa alishangazwa sana na mwanawe
ambaye alihatarisha maisha yake kwenda kumtafuta.
Alisema
kuwa tangu wanawe na baba yao kwenda Marekani,, amekuwa akijaribu sana
kuwatafuta bila mafanikio.
Baada
ya Yahya Abdi kupatikana akiwa katika uwanja wa kutua ndege aliambia mafisa wa
usalama kuwa alikuwa ametofautiana na famia yake nyumbani na ndio maana akaamua
kuchukua ndege ya kwanza aliyopitaka kurejea Somalia.
Katika
mahojiano na shirika la habari la Voice of America, babake kijana huyo Abdilahi
Yusuf Abdi, alisema kuwa Mungu alimuokoa mwanawe ambaye daima alikuwa anataka
kurejeaAfrika.
CHANZO BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment