Mshambulizi wa Liiverpool Luis Suarez,
ametajwa kuwa mchezaji mwenye tajriba na maarifa ya hali ya juu mwaka huu.
Suarez
mwenye umri wa miaka 27 alisafiri kuelekea katika sherehe hizo baada ya wao
kushindwa na timu ya Chelsea.
Suarez kufikia sasa amefunga
mabao 30 na ndiye anayeongoza matumaini Liverpool kukatisha ukame wa miaka 24
tangu watwae taji la ligi kuu ya Uingereza.
Suarez
atakumbukwa zaidi kwa kisa kilichogonga vichwa vya habari duniani baada ya
kumngata mchezaji wa Chelsea Branislav Ivanovic, Suarez alipigwa marufuku ya
mechi Kumi baada ya kupatikana na hatia .
Wengine walioteuliwa ni Eden
Hazzard wa Chelsea aliyetajwa kama mchezaji mchanga wa mwaka huu.
Daniel
Sturridge na naodha wa Liverpool Steven Gerrard walijiunga na Suarez kutokana
ushirikiano wao iliyopelekea Liverpool kutajwa kama klabu bora ya mwaka huu.
Waliokuwemo
ni pamoja na Kipa wa Chelsea Peter Czech na mlinzi Gary Cahil.
Hata
hivyo msururu huo haingekamilika pasipo kuwataja Yaya Toure na Vincent Kompany wote
wa Manchester City.
Luke
Shaw na Adam Lallan wa Southampton pia wakitajwa katika orodha hiyo naye Seamus
Coleman wa Everton akifunga ukurasa huo.
Akizungumuza
katika sherehe hiyo Suarez alisema kuwa. "‘Ligi ya Primia ina
wachezaji wengi ambao ni wazuri zaidi na ni jambo la heshima sana wachezaji
hawa wakiona mchango wako uwanjani’"
CHANZO BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment