Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 29 April 2014

ZIARA YA MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA, KATA YA KAWE YATIKISA

 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Taifa, Sadifa Juma (wapili kushoto) akiwasili kwenye Uwanja wa Mkutano eneo la Tanganyika Packers, Kawe Dar es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014 ambako mbali na kuhutubia mkutano wa hadhara, alikabidhi vifaa vya michezo kwa timu mbalimbali za soka katika kata ya Kawe. Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kawe, Lilian Rwebangila na Katibu wa UVCCM wa kata hiyo, Aisha Katundu na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Kata hiyo Said Herry.
 Vijana wa CCM na wananchi kwa jumla wakimsindikiza Sadifa, kwa hamasa kuingia uwanjani
 Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM (Bara) Mfaume Ali Kizigo akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa UVCCM uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe Dar es Salaam, Jumapili ya Aprili 27, 2014, kumkaribisha Sadifa kuhutubia.
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kawe Lilian Rwebangila akimkaribisha Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Hamis Juma, kuhutubia mkutano huo wa hadhara kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe.
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Hamis Juma, akihutubia mkutano wa hadhara huku shamrashamra zikitawala, kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Dar es Salaam, Jumapili Aprili 27, 2014.
Sadifa akigawa vifaa vya michezo kwa kiongozi wa timu ya soka ya Ukwamani Shooting, wakati wa mkutano huo
Mlezi wa UVCCM Kata ya Kawe, Coolman Massawe, akikabidhi vifaa vya michezo kwa kiongozi wa timu ya Ukwamani, Ali Kidogodogo, wakati wa mkutano huo
Sadifa (kushoto) akishuhudia wakati Katibu wa CCM wilaya ya Kinondoni, Athuman Shemsha, akimtawaza Kada wa CCM, Vincet Massawe, wakati wa mkutano wa hadhara wa UVCCM  uliofanyika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Dar es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamis akimwelekeza jambo, Kamanda wa UVCCM Kata ya Kawe, Vincent Masawe wakati wa mkutano huo
Kamanda wa UVCCM Kata ya Kawe, Masawe akishukuru kwa kupewa ukamanda huo. Kushoto ni Sadifa akimsikiliza
Katibu wa UVCCM Kata ya Kawe, Dar es Salaam, Aisha Kitundu (katikati) akiwa na Wasanii wa Kikundi cha TOT, Malkia wa Mipasho Nchini, Khadija Kopana na Jane Komba wakati wa mkutano huo
Vijana wa Kikosi kazi cha UVCCM Kata ya Kawe wakipozi kwa picha maalum ya kumbukumbu wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya viongozi wa CCM na UVCCM Kawe waliohudhuria kwenye mkutano huo. Kushoto ni Kamanda wa UVCCM Kawe,Aisha Voniatis na Mlezi wa Wazazi Muta Rwakatare

Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM (Bara) Mfaume Ali Kizigo akiwa na viongozi wa Chipukizi, Nimka Lameck (Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa) na Maleo Motelo (Mwenyekiti wa UVCCM Kinondoni) baada ya uzinduzi wa Tawi UVCCM la Kawe, Mnarani, Dar es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014.

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Hamis Juma akizindua Tawi la UVCCM, Kawe Mnarani, DSar es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014.
Kamanda wa UVCCM Kawe, akitoa mchango wa sh.  200,000 kwa Ktb wa tawi la UVCCM Mnarani, Mlangala Zacharia kwa ajili mradi wa maendeleo ya tawi hilo. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog

CHANZO,FULL SHANGWE 

No comments:

Post a Comment