Hukumu dhidi ya Muslim Brotherhood kutolewa.
Mahakama moja katika mji
wa Minya leo inatarajiwa kutoa uamuzi wake wa mwisho kuhusu hukumu ya kifo
iliyotolewa mwezi uliopita kwa wafuasi 529 wa vuguvugu la Muslim Brotherhood
ambalo sasa limepigwa marufuku nchini humo.
Kesi
hiyo ilizua shutuma kali kutoka jamii ya kimataifa.
Watu
hao walipatikana na hatia ya kumuua afisa mmoja wa polisi katika rabsha
zilizozuka mwezi Agosti mwaka uliopita.
Watu
hao walihukumiwa kifo kwa mara ya kwanza mwezi Machi baada ya kesi kufanyika kwa
takriban saa moja.
Mawakili
wa utetezi walinyimwa fursa ya kujieleza na hata mashtaka hayakutangazwa.
Baadaye
kesi hiyo iliwasilishwa mbele ya mmoja ya viongozi wakuu wa kidini ili
kuamuliwa tena lakini maoni yake hayakuzingatiwa.
Miongoni
mwa waliohukumiwa kunyongwa ni vijana wawili wenye umri wa miaka 17, mtu mmoja
mlemavu na wakili aliyewakilisha baadhi ya
washukiwa
hadi alipokamatwa.
Mawakili
wa washtakiwa wamesema watakata rufaa iwapo mahakama itapitisha hukumu
zilizotolewa.
Baadhi
ya wataalam wa maswala ya sheria wametabiri kuwa huenda kesi dhidi ya waku hao
ikasikizwa tena.
Mahakama
pia inatarajiwa kutoa uamuzi katika kesi ya pili dhidi ya watu 700 wanaoshukiwa
kuwa wafuasi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood
baadhi
wakikabiliwa na mashtaka ya kuhusika katika machafuko.
CHANZO, BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment