Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 27 April 2014

TAASISI ZA FEDHA ZASHAURIWA KUWAWEZESHA WAKULIMA

DC wa Arumeru, Nyerembe Munasa

Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot.com, Arusha

TAASISI  za kifedha zimetakiwa kangalia umuhimu  wa kwawezesha wakulima  kuwakopesha mikopo kwa kutumia dhamana ya hatimiliki za kimila ili waweze kulima kilimo cha biashara kwa kuwa ndio dhamana pekee wakulima waliyo nayo.
Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Nyerembe Munasa alipokuwa akifungua maonyesho ya kilimobiashara ya  kuwaunganisha wakulima na taasisi  kifedha  yanayofanyika katika viwanja vya AVRDC Tengeru mjini Arusha.
Munasa alisema kuwa asilimia kubwa ya ya wakulima wa vijijini wanategemea dhamana ya hati miliki za kimila katika kujipatia mikopo na hivyo taasisi zinapaswa kuhakikisha kuwa zinawawezesha wakulima hao kwa kuwapatia mokopo ili waweze kuendeleza kilimo chao kiweze kuwa cha manufaa zaidi.
Alieleza kuwa taasis zinazokataa kukopesha wakulima mikopo kwa kupitia dhamana ya hati miliki za kimila zinachangia sana kuwanyima wakulima kutofikia malengo yao ya kilimo cha biashara ambacho ndicho kinachotegemewa kwa sasa.
Aliongeza kuwa taasisi zozote za kifedha zinazokataa kuwawezesha wakulima kwa kupitia hati miliki za kimila zinavunja sheria na kwamba watakaobanika kukataa dhamana hiyo watakchukuliwa hatua za kinidhamu.
“Naombeni sana ninyi taasisi za kifedha wapeni wakulima mikopo kwa kutumia dhamana ya hatimiliki za kimila na ni makosa makubwa sana kuwanyima mikopo kwa dhamana hii maana ndio dhamana waliyo nayo,” alisistiza.
Awali Meneja Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania tawi la Arusha Wilfred Mbowe akizungumza na wakulima katika maonyesho  hayo alisema kuwa benki kuu itaendelea kushirikiana na wakulima kwa kuwapatia mikopo mbali mbali kwa kuwa ndio benki mama ambayo imezaa taasisi nyinginezo ambazo zimekuwa bega kwa began a wakulima .
Mbowe alisema benki hiyo itahakikisha kuwa inaendelea kutoa elimu kwa wakulima na hata pia kusisitizia taasisi nyinginezo umuhimu wa kushirikiana na wakulima ili kuhakikisha kuwa kilimo cha hapa Tanzania kinakuwa cha manufaa makubwa zaidi.
Naye Mkurugenzi wa Chama cha Wakulima wa Mboga mboga, Maua, Matunda na Viungo (TAHA) Jacquline Mkindi alisema kuwa maonyesho hayo yanachangia kuwapa wakulima fursa za kuwafanya waweze kukopa katika taasisi za kifedha kwa kuwa wakulima wengi wameshindwa kufikia malengo ya kilimo chao kutoka na kukosa mitaji ya biashara.
Alieleza kuwa kupitia maonyesho hayo wakulima watapata elimu na mbinu ambazo zitawafnya kilimo chao kuwa cha manufaa zaidi huku wakiwa wanapata hata pembejeo za kilimo chao kwa kupitia taasis hizo ambazo zitakuwa zinatoa mikopo kwa kupitia dhamana walizo nazo .

No comments:

Post a Comment