FT: TAIFA STARS 0: 3 BURUNDI
Dakika 45` za kipindi cha pili zimeshakatika na kuongezwa dakika 3.
Dakika ya 38 kipindi cha pili, stars wanapata kona na kukosa bao la wazi baada ya kazi nzuri ya Msuva na Omary Nyenje kushindwa kugusa mpira kuutumbukiza wavuni.
Dakika ya 35` kipindi cha pili, Stars wapo nyuma kwa mabao 3-0
Dakika ya 30` kipindi cha pili Burundi wanaongoza kwa mabao 3-0.
Dakika ya 25` kipindi cha pili, Taifa stars wapo nyuma kwa mabao 3-0 dhidi ya Burundi.
Dakika ya 19` kipindi cha pili, Taifa Stars inashindwa kumudu kabisa kasi ya Burundi, lakini Kocha Salum Mayanga amefanya mabadiliko yanayoonekana kuwapa uhai Stars.
Burundi wanaandika bao la tatu kupitia kwa Yusuf Ndikumana.
Amis Tambwe anaifungia Burundi bao la pili kwa shuti kali la chini chini lililomshinda kipa Deo Munish.
Dakika ya 9` kipindi cha pili kona inachongwa kueleka lango la Stars, lakini mabeki wanaokoa.
Didier Kavumbagu anadhihirisha kuwa kasi yake ya kufunga ni ileile.
Wachezaji wa Taifa stars hawana kasi kama wanavyocheza katika klabu zao. Sijui tatizo ni nini hapo uwanja wa Taifa.
Jonas Mkude, Harun Chanongo na Himid Mao wamenyanyuliwa na kuanza kupasha moto misuli.
Dakika ya 4` kipindi cha pili, Burundi bado wanaoongoza kwa bao 1-0.
Almanusura Burundi waandike bao la pili, lakini mpira unaokolewa na Dida na kuwa kona inayoondoshwa na Agrey Moris.
Mpira umeshanza hapa uwanja wa Taifa
Kipindi cha pili kinatarajia kuanza hivi punde, naona waamuzi na wachezaji wa akiba wakiingia uwanjani.
HT: TAIFA STARS 0: 1 BURUNDI
Dakika ya 45` kipindi cha kwanza, Didier Kavumbagu anaifungia Burundi bao la kuongoza.
DDakika ya 40` kipindi cha kwanza bao bila kwa bila.
Mpira umesimama hapa uwanja wa Taifa, kipa wa Stars, Deo Munish akiwa chini akigangwagangwa.
Dakika 31` za kipindi cha kwanza zimeshakatika, hakuna bao kwa timu zote.
Mohamed Seif anaikosesha bao Taifa stars kufuatia krosi ya Saimon Msuva.
Stars wanafanya shambulizi kali, lakini shuti alilopiga Saimon Msuva linakuwa mboga kwa kipa wa Burundi.
Dakika ya 16` kipindi cha kwanza hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.
Dakika ya 8` kipindi cha kwanza Burundi wanapata kona,lakini Ramadhan Singano `Messi` anaokoa.
Mpira umeshaanza uwanja wa Taifa
TAIFA STRS 0 VS 3 BURUNDI
CHANZO, MPENJA
No comments:
Post a Comment