Vurugu zinashuhudiwa nchini Sudan pande za kisiasa zikizozana kuhusu mamlaka
Mkuu wa shirika la Umoja
wa Mataifa la haki za binadamu , Navi Pillay yuko nchini Sudan kusini kutathmin
hali huko baada ya miezi minne ya mzozo .
Ziara
yake inakuja siku kadhaa tu baada ya watu wenye silaha kushambulia kambi ya
Umoja wa Mataifa iliyoko Bor, na kuwauwa takriban watu 58 wakiwemo wahudumu na
watoto .
Bi
Pillay atakutana pia na watu walioyahama makazi yao kutokana na vita. Juma
lililopita mamia ya raia waliuawa Bentiu-- mji mkuu wa jimbo lenye utajiri wa
Mafuta.
Waziri
wa mambo ya nje wa Sudan Kusini , Barnaba Mariel Benjamin ameiambia BBC kuwa
serikali yake inataraji Umoja wa Mataifa utalaani mauaji ya raia wanayolaumiwa
kuyafanya waasi.
Wakati
huo huo wawakilishi wa pande husika na mzozo huo wamerejea mjini Addis Ababa Ethiopia
kufufua mazungumzo ya amani.
CHANZO BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment