CARLO Ancelotti anaamini kuwa hali ya hewa iliyopo Real Madrid kwa sasa inatosha kuwapa ushindi dhidi ya Bayern Munich kesho kutwa (jumanne) kwenye nusu fainali ya pili ya UEFA uwanja wa Allianz Arena.
Ancelloti aliiongoza Real Madrid kuifunga bao 1-0 Bayern kwenye nusu fainali ya kwanza uwanja wa Santiago Bernabeu wiki iliyopita na bao hilo pekee lilifungwa na mfaransa, Karim Benzema.
Madrid walipasha moto misuli yao jana kwa kuifunga Osasuna mabao 4-0 kwenye mchezo wa La Liga na mabao hayo yalifungwa na Sergio Ramos, Daniel Carvajal na `Mnyama` Cristiano Ronaldo alipiga mawili.
“Ni wazi kujua hali ya hewa iliyopo sasa katika klabu na mashabiki wake”. Alisema Ancelotti mwenye miaka 54.
“Kama nisemavyo mara kwa mara, hii ni muhimu, ni muhimu kuwa na hali kama hii kuelekea mechi zijazo”.
Los Blancos (Real Madrid) wanapigania kuchukua kombe la UEFA kwa mara ya 10 tangu walipofanya hivyo mwaka 2002 walipoifunga mabao 2-1 Bayern Leverkusen.
Ancelotti amekaririwa akisema kwa kikosi chake cha sasa anataka kuwa meneja wa kwanza kuiongoza Real Madrid katika harakati zake za kuchukua kombe la UEFA kwa desimali mbili yaani 10.
“Kila mtu anasubiri kuona nini kitatokea na kwa mawazo haya klabu inaweza kufanya vizuri. Alisema Carlo.
“Kikosi nitakachopanga mjini Munich ni kile cha wachezaji wapambanaji. Kwasasa hatutafanya mabadiliko yoyote kuhusiana na mchezo huo”.
“Kila mtu awe mtulivu kwasababu tunajiandaa vizuri juu ya mechi hii. Nawaamini wachezaji wangu na nadhani kila mtu awaamini”. Aliongeza Carlo.
CHANZO, MPENJABLOG
No comments:
Post a Comment