Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Magereza, Deonice Chamulesile akisoma risala ya ufunguzi katika Kikao cha uwasilishaji wa Stadi juu ya jinsi ya kudhibiti idadi ya Wafungwa Magerezani iliyofanywa na Asasi ya Kiraia ya IRaWS – T. Kikao hicho kimefanyika leo Aprili 30, 2014 katika Ukumbi wa Luther House, Jijini Dar es Salaam(wa kwanza kulia) ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Nicas Banzi(wa pili kushoto) ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza Onel Malisa(wa kwanza kushoto) ni Katibu Mtendaji wa Asasi ya IRaWS – T, Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, John Nyoka.
Baadhi ya Watoa Mada mbalimbali wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa Stadi juu ya jinsi ya kudhibiti idadi ya Wafungwa Magerezani(kushoto) ni Afisa Mtafiti Mwandamizi toka Tume ya Kurekebisha Sheria, Prof. Sufian Bukurula.
Mhadhiri toka Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bw. James Jesey(aliyesimama) akiwasilisha rasmi Stadi ya jinsi ya kudhibiti idadi ya Wafungwa Magerezani.
Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau mbalimbali waliohudhuria Kikao hicho cha uwasilishaji wa Stadi juu ya jinsi ya kudhibiti idadi ya Wafungwa Magerezani. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Luther House, leo Aprili 30, 2014 Jijini Dar es Salaam(wa kwanza kulia) ni Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya IRaWS – TANZANIA, Kamishna Mkuu Mstaafu Magereza Nicas Banzi(wa pili kushoto) ni Mwenyekiti wa Asasi ya IRaWS – Tanzania, Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza Onel Malisa(wa kwanza kushoto) ni Afisa Mwandamizi Mstaafu wa Magereza, Bi Regina Thomas(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
CHANZO,FULL SHANGWE
No comments:
Post a Comment