Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot.com, Arusha
JAMII za wafugaji zimeaswa kuhakikisha kuwa zinajijengea tabia ya kutafuta na kutumia fursa nyingi za mikopo kwani tafiti zinaonesha kuwa wengi wana fursa ila wanashindwa kuzitumia na hivyo kusababisha umaskini kuongezeka kwa asilimia kubwa mwaka hadi mwaka.
Aidha kama jamii hizo za wafugaji zitaweza kutumia vema fursa za mikopo ambazo zipo kwenye taasisi za fedha basi zitachangia sana ongezeko la uchumi tofautiu na sasa ambapo bado wafugaji wengi wanakwepa mikopo hiyo.
Hayo yameelezwa na Afisa Ushirika Wilaya ya Longido ,Reginald Lyakurwa wakati akiongea na Wananchi Kitombeine mara baada ya shirika la World Vision kwa kushirikiana na Shirika la Vision Fund kutanga rasmi mradi wa mikopo kwenye jamii ya wafugaji hasa wa eneo hilo mapema jana.Aidha kama jamii hizo za wafugaji zitaweza kutumia vema fursa za mikopo ambazo zipo kwenye taasisi za fedha basi zitachangia sana ongezeko la uchumi tofautiu na sasa ambapo bado wafugaji wengi wanakwepa mikopo hiyo.
Lyakurwa alisema kuwa wafugaji wa sasa wanatakiwa kuachana na mila potofu za kukwepa mikopo na kisha kujiunga kwenye vikundi na kisha kukopa kwa ajili ya kuweza kunenepesha hata mifugo yao ambayo wakati mwingine hufa kutokana na ukosefu wa malisho.
Alisema kuwa kama watajiunga kwenye vikundi na kisha kukopa wataweza kufanya kazi ya ufugaji kuwa raisi sana na hivyo wataweza kufuraia kazi zao za ufugaji tofauti na sasa ambapo wengi wanatumikia mifugo
"Leo tumeweza kuleta fursa za mikopo hapa Kitombeine kuna fursa nyingi sana za mikopo ila hazitumiki sasa tunaomba wafugaji muweze kukopa na kisha hata muweze kunenepesha mifugo yenu ambayo kama itakuwa kwenye hali nzuri soko lipo karibu tu hapa Kenya ila kama mkiendelea kulea mifugo alafu ni dhaifu kwa kuwa hamna namna ya kuwasaidia ni wazi kuwa mtakuwa mnasumbuka sana na umaskini kamwe hauwezi kuisha"aliongeza Lyakurwa.
Wakati huo huo alidai kuwa kitu kikubwa ambacho kinawafanya wafugaji wengi washindwe kukopa ni kutokana na kuwa wengi bado wanafikra potofu juu ya mikopo hali ambayo wakati mwingine inachochea umaskini.
Naye Kaimu Mratibu wa mradi huo wa Mikopo katika eneo hilo Bw George Banyenza alisema kuwa mradi huo ni wa maendeleo na lengo lake halisi ni kuhakikisha kuwa wananchi wanaepukana na umaskini
Banyenza alisema kuwa waliweza kufanya tafiti kwa miaka mingi iliyopita na kisha kuweza kugundua kuwa endapo kama eneo hilo la Kitombeine litapata miradi ya kukopa basi litaweza kuwa balozi mzuri sana wa maendeleo kwa nchi za jirani
Alimalizia kwa kusema kuwa mradi huo utaweza kuwanufaisha wananchi zaidi ya 500 ambapo wataweza kupata fursa za mikopo na kisha kujinufaisha wao wenyewe na hata mifugo yao ambayo wanaitumia kama ajira kwenye maisha yao ya kila siku.
No comments:
Post a Comment