Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 27 April 2014

SHERIA DUNIANI, HAKI MBINGUNI!

Ndugu zangu,
Tangu Wana wa Israel walipoasi kwa Mungu baada ya kutoka Misri walikokaa utumwani kwa miaka 400, mambo yakabadilka duniani kwa sababu wanadamu wakaukosa utukufu wa Mungu.
Ndiyo maana Mungu akampatia Nabii Musa Torati (Sheria) ili kwazo wanadamu waenende nazo na watakapokuwa wamekosea, basi wahukumiwe kwa sheria hizo.
Hata hivyo, sheria hizi mara nyingi hazitendi haki hasa kwa wanyonge. Mwananchi wa kawaida anadhulumiwa haki yake kwa sababu anayegombana naye anayo fedha ya kuweza 'kuichezea' sheria.
Ndiyo maana, mahabusu na magereza zimejaa watu wasio na hatia wakati wahalifu wakubwa wanatembea uraiani wakipiga mluzi tu.
Kijana aliyeshikwa na kesi ya kuku anaozea jela, kigogo aliyekwiba mabilioni ya fedha za umma, anakula kiyoyozi.
Kweli, Sheria iko duniani, lakini itapatikana Mbinguni!

Daniel Mbega.

No comments:

Post a Comment