Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 29 April 2014

ANCELOTTI, GAURDIOLA WAOGOPANA KIAINA, ALLIANZ ARENA MOTO KUWAKA



CARLO Ancelotti amesema Real Madrid inahitaji kufunga mabao katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya pili ya  UEFA dhidi ya Bayern Munich leo Allianz Arena.


Los Blancos (Real Madrid) wataingia uwanjani wakiwa wanaongoza kwa bao 1-0 walilofunga kupitia kwa Karim Benzema katika mchezo wa kwanza uwanja wa Santiago Bernabeu.

Lakini Ancelotti amesisitiza kuwa licha ya timu yake kuwa na faida ya bao moja si sababu ya kuingia kwa kulinda na ameshawaambiwa wachezaji wake kuonesha dhamira ya kucheza fainali baada ya kupita zaidi ya muongo mmoja.

“Inawezekana kufuzu bila kufunga, lakini dhamira yetu ni kufunga.”.

“Tumefunga mabao mengi UEFA na La Liga na tunahitaji kufanya hivyo tena”. Ancelotti amewaambiwa waandishi wa habari.

“Tunaweza kucheza mifumo tofauti ya mpira, lakini kwa michezo mingi tunajaribu kushambilia “
“ Tutatumia faida ya kuwa na wachezaji walioimarika kimaumbo na kiufundi”.

“Tunajua mechi ya leo itakuwa ngumu sana. Tunacheza na timu kubwa tukiwa na faida ndogo, kwahiyo sisi sio wapumbavu na kamwe hatuwezi kuingia kwa kudhani tayari tumeshafuzu”.

Naye Kocha wa Bayern Munich, Josep Pep Guardiola amesema malengo yake ni kupindua matokeo ya kwanza na kusonga hatua ya fainali.

Gaurdiola alikiri ugumu wa mchezo huo, lakini alisema wameshajiandaa kushinda.
“Mimi nataka kushinda. Wachezaji wanataka kushinda na mashabiki wanataka kushinda”
“Kwa matarajio kama haya, lazima tuingie kwa nguvu moja”.

“Najua Real Madrid ni timu kubwa na siku zote nafurahi kucheza nusu fainali hasa na klabu kama hii. Itakuwa mechi ngumu lakini tutajitahidi kupata matokeo”. Alisema Gaurdiola.

CHANZO MPENJA BLOG

No comments:

Post a Comment