Jaji wa mahakama nchini
Misri, amewahukumu kifo watu 683 akiwemo kiongozi wa kundi la Muslim
Brotherhood Mohammed Badie.
Mawakili
wa watuhumiwa wanasema kuwa wateja wao walikabiliwa na makosa mengi yakiwemo,
kushambulia kituo cha polisi mjini Minya mwaka 2013 ambapo polisi mmoja
aliuawa.
Jaji
huyo pia alibatilisha hukumu ya kifo iliyotolewa kwa watu 492 kati ya watu 529.
Hukumu hiyo ilipitishwa mwezi Machi na sasa watahudumia kifungo cha maisha
jela.
Kesi na
kasi ya kuzisikilizwa kwa kasi hizo, imesababisha hasira na kukosolewa na
shirika la kutetea haki za binadamu la Umoja wa Matifa UN.
Kadhalika
shirika la Huma Rights Watch limelalamika kuwa kesi hizo zilisikilizwa tu kwa
saa chache huku mahakama ikiwazuia mawakili kuwawakilisha washitakiwa.
Duru
zinasema kuwa jamaa wa watuhumiwa waliokuwa wanasubiri nje ya mahakama
walizirai baada ya kupokea taarifa za hukumu hiyo.
Mwezi
jana shirika la kutetea haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, lililaani kesi
hizo likisema kuwa zinakiuka sheria ya kimataifa ya haki za binadamu.
Msemaji
wa shirika hilo, Navi Pillay, alisema kuwa kesi hiyo ilikumbwa na makosa mengi
ya utarataibu.
Maafisa
wa utawala nchini Misri wamekuwa wakiwasaka na kuwakamata wapiganaji wa
kiisilamu na wanachama wa vuguvugu la Muslim Brotherhood ambao walimuingiza
mamlakani aliyekuwa Rais Mohammed Morsi ambaye baadaye aliondolewa na Julai.
Mamia
wameuawa huku maelfu ya raia wakikamatwa.
No comments:
Post a Comment