Miongoni
mwa maswala muhimu yatakayojadiliwa ombi la Sudan Kusini kutaka kujiunga na
jumuiya hiyo.
Mkutano
wa mwisho kama huu uliofanyika mjini Kampala Uganda mwezi Novemba mwaka jana,
uliweka bayana kwamba ni katika mkutano huuu wa Arusha, ambapo tarehe ya Sudan
Kusini kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki itakapotangazwa.
Lakini
wadadisi wanasema kuwa msukosuko wa kiuchumi pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe
huenda ikawa sababu ya taifa hilo kunyimwa uanachama wa jumuiya hiyo. Hii ni
baada ya machafuko ya wenyewe kwa wenyewe kuzuka, na kusambaratisha nchi hiyo
kisiasa na kiuchumi.
Maswala
mengine yatakayojadiliwa ni ripoti ya mawaziri, mikakati ya kifedha katika
kuiendesha jumuiya hiyo na mbinu za nchi wanachama kuendelea kupeana taarifa za
kijasusi, katika juhudi za kupambana na tishio la ugaidi.
CHANZO, BBCSWAHILI.
No comments:
Post a Comment