Uchaguzi kufanyika Iraq
Wapiga kura nchini Iraq
wanashiriki katika zoezi la upigaji kura katika mikoa yote isipokuwa mkoa mmoja
katika uchaguzi wa kwanza wa wabunge tangu wanajeshi wa Marekani waondoke
nchini humo mwaka 2011.
Waziri
mkuu wa sasa Nouri al-Maliki anagombea kiti chake kwa muhula wa tatu lakini
kampeni zimekuwa zikipigwa kwa misingi ya vurugu za kisiasa zinazoendelea
kukithiri nchini humo.
Selikali
ya muungano ya bwana Maliki inayoongozwa na chama cha Kishia imekabiliwa na
wakati mgumu kupambana na uasi unaongozwa na kundi lenye ufungamano na Al Qaeda
katika mji wa Falluja na mkoa wa Anbar.
Sauti
za mizinga zimekua taswira ya kila siku katika baadhi ya maeneo ya Iraq wakati
kampeni za kuelekea uchaguzi huu.
Matokeo
yake ni mashambulio ya kujitolea mhanga karibu kila siku.
Helikopta
za kijeshi zinashika doria katika anga ya Baghdad na serikali imefunga uwanja
wa ndege na baadhi ya barabara kuu ndani na nje ya mji huo.
Hatua
hizo zinanuia kuwapa imani wapigaji kura watakaojitokeza kwani ni bayana kuwa
huenda vituo vya kupigia kura vikalengwa.
Watu
160 wameuawa wiki iliyopita huku wengine 275 wakijeruhiwa.
Baadhi
ya taarifa zinaeleza kuwa vikosi vya usalama vimepoteza maafisa elfu moja mwaka
huu kwenye mapigano ya kukabiliana na uasi katika maeneo ya Fallujah na Anbar.
Inatabiriwa
kuwa huenda Bw Maliki akashinda awamu ya tatu na kumuwezesha kuunda serikali ya
muungano lakini ni bayana kuwa swala la usalama litasalia kuwa changamoto
kubwa.
CHANZO BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment