Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 27 April 2014

‘USHIRIKINA’ WAKWAMISHA MAPAMBANO YA MIMBA KWA WANAFUNZI MBEYA VIJIJINI

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Usoha Njiapanda iliyopo Mbeya Vijijini.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Usoha Njiapanda iliyopo Mbeya Vijijini.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Usoha Njiapanda, , Willson Mwamunyila (katikati) akizungumza na mwandishi wa habari hizi kijijini kwake.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Usoha Njiapanda, , Willson Mwamunyila (katikati) akizungumza na mwandishi wa habari hizi kijijini kwake.
Baadhi ya wanakijiji wa Kijiji cha Usoha Njiapanda wakiwa katika mkutano na mwanahabari hizi.
Baadhi ya wanakijiji wa Kijiji cha Usoha Njiapanda wakiwa katika mkutano na mwanahabari hizi.
VITISHO na hofu ya vitendo vya ushirikina imebainika kuwa vikwanzo vya mapambano ya baadhi ya watu wanaowatia mimba wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika Kata ya Tembela Wilaya ya Mbeya Vijijini, mkoani Mbeya. Kauli hiyo ilitolewa juzi mjini hapa na baadhi ya wanakijiji kutoka katika baadhi ya vijiji vya Kata ya Tembela walipofanya mahojiano kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi alipotembelea vijiji hivyo.
Akizungumza mkazi wa Kijiji cha Usoha Njiapanda, Maria Kolneri alisema baadhi ya wazazi hushindwa kuwawajibisha watu waliowatia mimba wanafunzi kwa kuhofia usalama wao kwani familia iliyotuhumiwa hujenga uhasama na familia ya mwanafunzi na hata kutoa vitisho. Alisema katika kijiji hicho ni vigumu kwa familia ya mwanafunzi aliyetiwa mimba kufuatilia ili sheria ichukuwe mkondo kwani huwa kuna vitisho na vingine kutoka kwa majirani wa familia hizo.
“…Hapa ukianza tu kumfuatilia mtu aliyefanya kosa kama hilo unasikia wanakijiji wanaanza kulalamika anataka kumfunga mwenzake sasa mtoto atakaye zaliwa atalelewa na nani…? Watakusema huku familia yenye kosa ikitoa vitisho hadi utaacha kufuatilia,” alisema.

“Ukitaka kupata kesi (uhasama) hapa kijijini kwetu mfunge kijana aliyempa mimba mtoto wako…, kila mwanakijiji anayekujua atakuona hufai kwa madai kuwa umemwonea kijana uliyemshtaki,” alisema mama huyo.

Aidha aliongeza kuwa baadhi ya familia uhofia vitendo vya ushirikina (kulogwa) endapo utaendelea kufutilia kesi za mimba hivyo kukata tamaa, jambo ambalo kwa sasa kijijini hapo limekuwa la kawaida.
Naye Nazareti Kibaga mkazi wa Kijiji cha Simambwe alisema kutokana na hali hiyo wananchi wamekuwa wagumu kufuatilia kesi za mimba jambo ambalo limefanya matukio hayo kuendelea licha ya changamoto zingine zinazochangia uwepo wake.

“…Hali hii imefanya mimba ziendelee na hakuna kesi yoyote dhidi ya wanaowatia mimba wanafunzi…, wazazi hawawajibiki, wananchi hawawajibiki na viongozi nao hawawajibiki,” alisema Kibaga.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Usoha Njiapanda, Willson Mwamunyila alikiri uwepo wa matukio ya mimba kwa kiasi kikubwa kijijini hapo lakini alisema kikwazo katika kushughulikia matukio ya mimba ni uongozi kukosa ushirikiano kutoka kwa wazazi na mwanafunzi.
“…Matatizo ya mimba yapo lakini wazazi na wanafunzi waliotiwa mimba hugoma kutoa ushirikiano kwa viongozi ili wahusika washughulikiwe kisheria. Unakuta mtoto kapata mimba baada ya taarifa kukufikia unaenda kwa mzazi wa mwanafunzi kuomba ushirikiano lakini wazazi wengine wanakuzunguka wanazungumza na mwalimu kwenye shule husika na wanamalizana wenyewe,” alisema Willson Mwamunyila.

CHANZO, FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment