Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 27 April 2014

TASWA KUSHIRIKI MKUTANO MKUU WA 77 WA AIPS

amir mhando(TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI)

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinatarajia kushiriki kwenye Mkutano Mkuu wa 77 wa Chama cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS) unaotarajiwa kuanza kesho (Jumapili) jijini Baku, Azerbaijan hadi Mei mosi mwaka huu.

Mkutano huo wa kawaida wa mwaka utashirikisha viongozi wa  vyama vya waandishi wa habari za michezo zaidi ya 150 duniani ambao ni wanachama wa AIPS na pia kutafanyika mikutano ya mabara ya vyama vya waandishi wa habari za michezo, ambao pia TASWA itashiriki upande wa bara la Afrika.

Pamoja na mambo mengine kutaendeshwa semina kuhusiana na masuala mbalimbali ya kuwaendeleza waandishi wa habari za michezo na pia utajadili changamoto zinazoikabili tasnia ya habari hasa wakati huu wa kukua kwa kasi kwa sayansi na teknolojia pamoja na mitandao ya kijamii.

Katika mkutano huo, TASWA itawakilishwa na Katibu Mkuu, Amir Mhando ambaye anatarajiwa kuondoka leo (Jumamosi) jioni kwa ndege ya Qatar Airways akipitia Doha, Qatar.

TASWA inamshukuru sana Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa kugharamia tiketi ya Katibu Mkuu kwenda na kurudi katika mkutano huo na hiyo inaonesha namna gani taasisi hizo mbili zinavyofanya kazi kwa kushirikiana.

Chama chetu ni mwanachama hai wa AIPS yenye makao yake makuu Lausanne, Uswisi, ndiyo sababu kila mwaka tumekuwa tukishiriki mikutano ya namna hiyo, ambayo hushirikisha viongozi wa juu wa nchi wanachama.

Ahsanteni.
Grace Hoka
Kaimu Katibu Mkuu (0718 722626)

CHANZO, MPENJA 


No comments:

Post a Comment