Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 30 November 2014

ONGEZENI UZALENDO KUKUZA ELIMU - LAIZER


Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny BlogArusha: JAMII imeaswa kuhakikisha kuwa inaongeza kiasi kikubwa cha uzalendo hasa kwenye sekta ya elimu kwani kwa sasa wapo baadhi ya watu kwenye jamii ambao bado hawajajua madhara na faida za kupata au kukosa elimu.

ONGEZENI UZALENDO KUKUZA ELIMU - LAIZER


Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny BlogArusha: JAMII imeaswa kuhakikisha kuwa inaongeza kiasi kikubwa cha uzalendo hasa kwenye sekta ya elimu kwani kwa sasa wapo baadhi ya watu kwenye jamii ambao bado hawajajua madhara na faida za kupata au kukosa elimu.

ONGEZENI UZALENDO KUKUZA ELIMU - LAIZER


Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny BlogArusha: JAMII imeaswa kuhakikisha kuwa inaongeza kiasi kikubwa cha uzalendo hasa kwenye sekta ya elimu kwani kwa sasa wapo baadhi ya watu kwenye jamii ambao bado hawajajua madhara na faida za kupata au kukosa elimu.

WANAFUNZI 826 NA WALIMU WAO WAKIMBIA VITA KITETO

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na wananchi baada ya mapigano baina ya wakulima na wafugaji mapema mwaka huu.

Na Mussa Juma, Mwananchi
Siku kadhaa zimepita tangu kutokea kwa mapigano mapya kati ya wakulima na wafugaji katika Wilaya ya Kiteto, mkoani Manyara.

WALIOKUFA KWA EBOLA WAFIKIA 7,000

Guinea
Takwimu mpya zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani, WHO, zinaonesha kuwa watu karibu 7,000 wamefariki hadi sasa kutokana na Ebola, karibu wote Afrika Magharibi.

RAIS KIKWETE ASEMA AMEPONA SARATANI

Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake kwa Taifa baada ya kurejea kutoka Marekani jana.
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema amepona saratani baada ya kufanyiwa upasuaji mapema mwezi huu nchini Marekani.

STANBIC BANK LOSES SHS. 800 MILLION IN FAKE DOLLAR SCAM


By  IVAN OKUDA & CHRIS OBORE
Kampala- Stanbic Bank has suspended four employees in connection with a sophisticated fraud scheme in which the bank was fleeced of $317,000 (about Shs800m) that was drawn by eight people in just four days.

KINANA AFANYA ZIARA MTWARA MJINI NA KUWATAKA WANA-CCM KUSHIKAMANA


 Vijana wa Bodaboda wakiongoza msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akiwasili Mtwara mjini ambapo alishiriki shughuli mbali mbali za kujenga na kuimarisha chama pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.

Saturday 29 November 2014

HAYA NDIYO MAAZIMIO YA BUNGE SAKATA LA ESCROW: HATMA YA PINDA, MUHONGO MIKONONI MWA KIKWETE!

MAAZIMIO YA BUNGE KUHUSU HOJA YA TAARIFA MAALUM YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI KUHUSU TAARIFA YA UKAGUZI 
MAALUM KUHUSIANA NA MIAMALA ILIYOFANYIKA KATIKA AKAUNTI YA ‘ESCROW’ YA TEGETA
PAMOJA NA UMILIKI WA KAMPUNI YA IPTL
_____________________________________

1.    KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuhusu Ukaguzi Maalum wa Malipo yaliyofanyika katika Akaunti ya Escrow ya Tegeta uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (‘CAG’) pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (‘TAKUKURU’) imeonesha kwamba kwamba Harbinder Singh Sethi, James Rugemalira (VIP), Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Waziri wa Nishati na Madini, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (‘TANESCO’) walihusika kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha kufanyika miamala haramu ya fedha za Akaunti ya Escrow ya Tegeta kwenda kwa makampuni ya Pan African Power Solutions Ltd. (‘PAP’), na VIP Engineering & Marketing (‘VIP’);

CHINA YAFANYA SHEREHE YA MIAKA 50 YA UHUSIANO NA TANZANIA

 Mkuu wa Msafara wa Kikundi cha Sanaa cha Nanjing kutoka China akihutubia kwenye sherehe hizo.

KASHFA YA ESCROW: TAARIFA YA BENKI YA MKOMBOZI KWA UMMA

TAARIFA YA BENKI YA MKOMBOZI KWA UMMA
Utangulizi
Taarifa hii inatolewa kwa umma kutokana na ripoti mbalimbali zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari mitandao ya kijamii na taarifa iliyotolewa kwenye mjadala katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
1. Ufunguzi wa akaunti ya VIP Engineering and Marketing (VIP)
Kampuni ya VIP engineering and Marketing ni kampuni ambayo imesajiliwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Kampuni hii ilifungua akaunti katika benki ya biashara ya Mkombozi na hivyo kuwa moja kati ya wateja wa benki. Benki ilijiridhisha na ilizingatia taratibu zote za ufunguzi wa akaunti husika kwa kuzingatia sheria za nchi na kanuni zinazozitaka benki kupata nyaraka muhimu kutoka kwa mteja wakati wa ufunguzi wa akaunti hiyo.

TANDIKA VICOBA GROUP YALIVYOZINDULIWA RASMI DAR JANA NOVEMBA 28-2014

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB), Margareth Chacha (kulia), pamoja na Mwenyekiti wa Tavico, Sarah Chikuni wakikata keki maalumu ya uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya Kanisa Katoliki la Chang'ombe Dar es Salaam jana.

HELIKOPTA YAANGUKA UKONGA , 4 WAPOTEZA MAISHA

 Ndege aina ya Helikopta ikiwa na Abiria 4 imeanguka jirani kabisa na Moshi Bar eneo la Sukuma Land Bar Ukonga. Abiria wote Askari wa Jeshi la Polisi wamepoteza maisha papo hapo.

HII SASA NI HATARI, BUNGE LAAHIRISHWA MARA MBILI KUTAFUTA MUAFAKA MAAZIMIO YA PAC

Spika Ane Makinda

Dodoma. Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania limeongeza muda wake na kusitisha vikao vyake mara mbili ili kutafuta muafaka juu ya andikaji wa maazimio yatakayotumiwa kuwawajibisha wale wote waliohusika na kashfa ya Escrow.

BAN KI MOON ASTUSHWA PROFESA TIBAIJUKA KUHUSISHWA KASHFA YA ESCROW

Ban Ki Moon, Katibu Mkuu wa UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki Moon, ameshtushwa na tukio la Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Kazi, Profesa Anna Tibaijuka kuhusishwa wizi wa mabilioni ya shilingi unaosadikiwa kufanywa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.

LOWASSA AKANUSHA KUANZISHA MTANDAO AKAUNTI YA ESCROW

Mhe. Edward Lowassa

Mbunge wa Monduli, Edward  Lowassa, amelaani kikundi cha watu kilichoanzisha ukurasa wa mtandao wa Twitter kwa kutumia jina lake unaohusu suala la Akaunti ya Escrow.

HALI YA HEWA YAENDELEA KUWANOA WATAALAMU WAKE KATIKA KUKIDHI VIGEZO VYA SHIRIKA LA HALI YA HEWA DUNIANI (WMO)

Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi ambaye pia alikuwa mgeni rasmi akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya huduma za hali ya hewa kwa ajili ya usafiri wa anga kutoka Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma.

KESI DHIDI YA HOSNI MUBARAK YATUPILIWA MBALI

Aliyekuwa Rais wa Misri, Hosni Mubarak
Mahakama moja nchini Misri imetupilia mbali kesi dhidi ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Hosni Mubarak kutokana na mauaji ya mamia ya waandamanaji wakati wa maandamano ya kumng'atua mamlakani.

HENRY ATAKA KUISAIDIA ARSENAL

Thierry Daniel Henry
Uwezekano wa Thiery Henry kujiunga na Arsenal kama mkufunzi umeongezeka baada ya mchezaji huyo wa Ufaransa kufichua kwamba bado ana ndoto ya kuisadia Arsenal kushinda taji la kilabu bingwa barani Ulaya.

SWAPO YAELEKEA KUSHINDA TENA NAMIBIA

Uchaguzi  mkuu wa Namibia
Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi mkuu wa Namibia yanaonesha kuwa chama tawala cha SWAPO kimeshinda kwa kura nyingi.

ABDULRAHMAN KINANA AENDELEA NA ZIARA MTWARA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumpokea wakati akiwasili wilaya ya Mtwara Vijijini.

Friday 28 November 2014

IKULU YA TANZANIA YAHUSISHWA NA KASHFA YA ESCROW


Bunge la Tanzania hapo jana liliambiwa kwamba afisa mmoja wa ikulu ya rais bwana Prosper Mbena aliandika barua ili kushinikiza hatua ya kutolewa kwa billioni 306 fedha za Escrow kutoka banki kuu ya Tanzania.

MTOTO MCHANGA ANUSURIKA KUUAWA KENYA



Mtoto X amelala kwa utulivu, akiwa amefunikwa na Blanketi lenye kumpa joto na kukumbatiwa na Mama yake katika Nyumba moja ya kulelea Watoto yatima nchini Kenya.

GBAGBO ATEULIWA KUWANIA URAIS AKIWA ICC

Laurent Gbagbo
Aliyekuwa Rais wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, anayezuiliwa katika mahakama ya kimataifa ya ICC, ameteuliwa kama mgombea mkuu wa Urais wa chama cha kisiasa alichokuwa anaongoza, kabla ya kuzuiliwa katika mahakama ya ICC.

MSIKITI WASHAMBULIWA NCHINI NIGERIA

Taarifa kutoka mjini Kano, Kaskazini ya Nigeria, zinasema kuwa watu wengi wamefariki na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la bomu.

MAELEZO YA SERIKALI KUHUSU TAARIFA YA UKAGUZI MAALUM KUHUSIANA NA MIAMALA ILIYOFANYIKA KATIKA AKAUNTI YA “ESCROW” YA TEGETA PAMOJA NA UMILIKI WA KAMPUNI YA IPTL

1.  Historia ya Mradi
 
Mheshimiwa SpikaKatika miaka ya tisini (1990s), Tanzania ilikuwa ikikabiliwa na tatizo la uhaba wa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme, hali iliyopelekea kuwepo kwa upungufu wa umeme na kuathiri shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini. Ili kukabiliana na tatizo hilo, Serikali ilichukua hatua za dharura za kuanzisha mradi wa kufua umeme wenye uwezo wa kuzalisha Megawati (MW) 100.

NYALANDU APIGA MARUFUKU UCHIMBAJI NDANI YA HIFADHI

Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu.

Na Cynthia Mwilolezi, Arusha
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amepiga marufuku uendeshaji wa shughuli za uchimbaji madini ndani ya hifadhi za taifa nchini na kuagiza walinzi wa hifadhi hizo kukamata watu wote watakaoingia  ndani ya hifadhi hizo kwa shughuli hizo.

WAKILI MKONO KALIPWA NA TANESCO SHS. 62.9 BILIONI

Nimrod Mkono 
Na Boniface Meena, Mwananchi
Dodoma. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema Kampuni ya Uwakili Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams ya Marekani imejiingizia Sh62.9 bilioni kwa ajili ya kuendesha kesi mbalimbali za Tanesco na IPTL hadi Septemba mwaka jana.

MAHAKAMA YAMTAKASA SHEIKH PONDA

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda 
Na James Magai, Mwananchi
Dar es Salaam. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemtakasa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda dhidi ya hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyomtia hatiani katika kesi ya jinai iliyotokana na mgogoro wa ardhi wa Chang’ombe Markazi.

ESCROW NJIAPANDA, WABUNGE WAGAWANYIKA

Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Msangi (katikati)  akiwasihi Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (kushoto) na Mbunge wa  Nkasi, Ali Kessy wasigombane kwenye Viwanja vya Bunge, mjini Dodoma jana. Picha na Emmanuel Herman 
Na Boniface Meena, Mwananchi
Dodoma. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo jana alipangua hoja zilizotolewa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), kuhusu ufisadi uliofanyika katika Akaunti ya Tegeta Escrow na kuacha wananchi njia panda kwa kutokuelewa nani anasema ukweli kati yake na kamati hiyo, inayoongozwa na Zitto Kabwe.

SADC ESSAY WRITING COMPETITION FOR SECONDARY SCHOOLS, 2015


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

MINISTRY OF EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING

SADC ESSAY WRITING COMPETITION FOR SECONDARY SCHOOLS, 2015

The Southern African Development Community (SADC) Secretariat has organized the SADC students essay writing competition for year 2015. The Essay writing competition is intended to broaden knowledge of the secondary school going population on SADC activities. The competition is open to form 1 to form 6 students. The students are required to begin researching on the topic prior writing and submitting to their Heads of School.

LAMUDI TANZANIA KUTANGAZA HUDUMA ZA MADALALI BURE

Meneja Huduma kwa Wateja wa Lamudi Tanzania, Godwin Lemma akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam. Meneja Huduma kwa Wateja wa Lamudi Tanzania, Godwin Lemma akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.

KAMPUNI ya Lamudi Tanzania, imetambulisha huduma yake ya kuwawezesha madalali mbalimbali wanaofanya kazi ya kuwatafutia nyumba, viwanja na magari wateja wao ili kuweza kutangaza huduma wanazotoa. 

COASTAL UNION U-20 KUCHEZA NA KOROGWE UNITED KESHO


NA MWANDISHI WETU, TANGA

TIMU ya Coastal Union U-20 ya Tanga Kesho  Inatarajiwa kusafiri kuelekea wilayani Korogwe mkoani Tanga kucheza mechi ya kirafiki na Mabingwa wa soka wilaya ya Korogwe,Korogwe United mechi itakayochezwa uwanja wa Chuo cha Ualimu wilayani humo.

TAARIFA YA VIP ENGINEERING AND MARKETING LTD: UMILIKI WA FEDHA ZA ESCROW HAUNA UTATA, TATIZO NI MAWAKILI

Mmiliki wa kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira, akiwa amemuinua mkono Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.

Kinachoitwa kwamba ni kashfa ya akaunti ya Escrow ni ngoma ambayo wanaoichezesha wanafanya hivyo kwa matumaini kwamba wakiivutia kwao basi hatimaye watafaidika ipasavyo. Miongoni mwa wanaoishangilia ngoma hii ni baadhi ya mawakili waliokuwa wakiitetea Tanesco na Benki ya Standard Chartered.

NI GHARIKA KUU TANZANIA, RICHMOND INA NAFUU!

Waziri Mkuu Mizengo Pinda

Gharika la ‘Tegeta Escrow’ limeikumba serikali baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na viongozi waandamizi kadhaa wa serikali kubainika kuhusika katika sakata la uporwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 ya fedha katika akunti hiyo iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

‘HII NDIYO SABABU YA KUFUNGULIWA ESCROW’



Na Fidelis Butahe, Mwananchi
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe ameanika chanzo cha kufunguliwa kwa Akaunti ya Tegeta Escrow kuwa ni mgogoro ulioibuka kati ya Tanesco na IPTL.

WAZIRI MUHONGO ASEMA FEDHA ZA ESCROW SI MALI YA UMMA, ADAI BADO SERIKALI INADAIWA

Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo 
Na Mwandishi Wetu, Mwananchi
Dodoma. Sakata la uchotwaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow linaendelea kuchukua sura mpya baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo kutoa ufafanuzi wa Serikali bungeni mjini Dodoma kuwa fedha hizo si za umma na kwamba bado Serikali ina mzigo wa madeni katika sakata hilo.

PHILIP HUGHES AFARIKI KWA KUPIGWA NA MPIRA, PELE ANA NAFUU

Philip Hughes alifariki jana kwa kupigwa na mpira

Bendera zinapepea nusu mlingoti katika viwanja vya cricket nchini Australia katika kuomboleza kifo cha mcheza cricket Philip Hughes aliyefariki jana baada ya kupigwa na mpira. 

MABOMU YARINDIMA NIGERIA, WATU WASHIKWA NA TAHARUKI

Wananchi wakiwa na taharuki ya mabomu
Watu wapatao ishirini na watano wamekufa kufuatia shambulio la bomu katika jimbo la Adamawa Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

MAELFU YA DOLA KUUKARABATI MJI WA BRISBANE

Mvua kubwa ikinyesha jijini Brisbane
Mji wa Brisbane nchini Australia umekumbwa na dhoruba mbaya kuwahi kutokea katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.

NJOO TUAGE MWEZI NOVEMBA KWA STAILI YA AINA YAKE NA SKYLIGHT BAND IKIWEMO RED CARPET TREATMENT, IJUMAA HII THAI VILLAGE

DSC_0016
Kutoka kushoto ni Dinga Mbepera, Aneth Kushaba AK47, Sam Mapenzi na Bella Kombo wakitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki ambapo ratiba ya Skylight Band wiki hii tukifunga mwezi Novemba kwa mwaka 2014 ni kama ifutavyo.

DK. TITUS KAMANI AZINDUA MRADI WA UFUGAJI WA SAMAKI NDANI YA ZIWA VICTORIA, KITEULE CHA BULAMBA WILAYANI BUNDA

Mgeni Rasmi Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (wa tatu kushoto) pamoja na wageni wengine waliohudhuria Sherehe hizo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Uchumi, Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Felix Samilani, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Raphael M. Muhuga, Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe. John Henjewele, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara, na Mkuu wa Kiteule cha Bulamba Meja David Msakulo.unnamed2Mgeni Rasmi Waziri wa Maendeleao ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (MB) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa Ufugaji wa Samaki ndani ya Ziwa Viktoria Kiteule cha Bulamba kwa kutumia teknolojia mpya ya vizimba (Cages). Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe.John Henjewele, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael M. Muhuga.unnamed3Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani akipandikiza vifaranga vya samaki ndani ya Ziwa Victoria, mradi unaotekelezwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilaya ya Bunda, Kiteule cha Bulamba kwa kutumia teknolojia mpya hapa nchini ya kuzalisha samaki kwenye vizimba.
unnamed4Picha ya vizimba ambavyo ufugaji wa samaki umeanza mara baada ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kuzindua mradi huo na kupandikiza vifaranga vya samaki. Mradi unatekeleza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilaya ya Bunda, Kiteule cha Bulamba kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Economic Social Research Foundation (ESRF), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Ufugaji wa samaki kwa kutumia teknolojia ya vizimba ndani ya Ziwa Victoria, umekuwa ukitekelezwa pia na wenzetu wa Kenya na Uganda ambao wamepiga hatua kubwa .
unnamed6Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP),  Mratibu Mwandamizi wa Mradi Bw. Nehemia Murusuri (wa kwanza kulia) pamoja na Mwakilishi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Mratibu wa Mradi wa Kuondoa Umaskini, Kukuza Uchumi na Utunzaji Endelevu wa Mazingira, Bw. Telesphory Kamugisha (wa pili kulia). Wengine ni baadhi ya wageni waliohudhuria sherehe hizo.unnamed7Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael M. Muhuga akiongea na wananchi wa Kijiji cha Bulamba wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Ufugaji wa samaki katika Ziwa Victoria kwa kutumia teknolojia ya vizimba (Cages) ambayo ni teknolojia mpya ndani ya nchi yetu.unnamed8Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani akitoa hotuba kwa wananchi wa kijiji cha Bulamba (hawapo pichani) mara baada ya kuzindua Mradi wa Ufugaji wa Samaki ndani ya Ziwa Viktoria. Aliwasisitiza wananchi kujiunga katika vikundi ili kujijengea uwezo wa kuanza kutumia teknolojia ya kisasa ya kuzalisha samaki kwa kutumia vizimba (Cages) katika ziwa Victoria.unnamed9Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (mwenye Kaundasuti nyeusi) akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma ya asili mara baada ya uzinduzi wa mradi huo. 

MATUKIO YA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA

1-spika wa makinda akitoa maelezo 
Spika wa Bunge Anne Makinda akitoa ufafanuzi hali iliyotokea Bungeni leo bungeni .Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)

BALOZI WA TANZANIA NCHINI CANADA AKUTANA NA DK. SHEIN

unnamedRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi Mpya wa Tanzania Nchini Canada Jack Mugendi Zoka alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha leo kwa Rais baada ya kuteuliwa rasmi.[Picha na Ikulu.]

MWANAMUZIKI BILEKU MPASI KUTOKA CONGO (DRC) NA MASHUJAA BAND KUFANYA ONESHO LA PAMOJA DESEMBA 12, 2014 UKUMBI WA TEN LOUNGE VICTORIA DAR


Rais wa Band ya Mashujaa, Chalz  Baba  

KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ARUSHA LEO