Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog
ARUSHA: SERIKALI imesema kuwa pamoja na kuwa madini aina ya Tanzite yanazalishwa nchini asilimia ishirini pekee ndiyo inayonufaisha Nchi huku asilimia 80 ikinufaisha nchi nyingine ikiwemo Kenya.
Hataivyo nchi ya Tanzania ina nufaika na asilimia hizo ishirini pekee kutokana na madini hayo kusafirishwa kwa kutumia njia za panya hali ambayo inachangia kwa kwa kiwango kikubwa umaskini
Hayo yameelezwa na Paul Masanja ambaye ni kamishna wa madini wakati akiongea na wadau wa madini kutoka katika nchi mbalimbali duniani kwenye uzinduzi wa maonesho ya tatu ya vito vya thamani jijini hapa mapema jana
Masanja alisema kuwa ni lazima sasa Serikali iweze kukiri kuwa hainufaiki na madini aina ya Tanzanite kwa kuwa asilimia nyingi zina nufaisha nchi nyingine tofauti na walengwa wa madini hayo
Akitolea mfano Masanja alisema kuwa takwimu zinaonesha kuwa nchi ya Kenya kwa kipindi cha mwaka jana pekee waliweza kuingiza kiasi cha dola za kimarekani milioni mia moja, huku nchi nyingine kama nchi ya India nayo ikingiza kiasi cha dola Milioni mia tatu, ambapo kwa Tanzania ambayo ndiyo yenye tanzanite nayo ikiingiza kiasi cha dola milioni thelathini na nane pekee hali ambayo si nzuri ukilinganisha na kitovu cha madini hayo.
“kwa hili hatuna ujanja ni lazima tukiri kuwa upotevu ni mkubwa sana na haya madini hayatunufaisha hata kidogo ila ukienda kwenye nchi zilizo endelea unakutana na madini haya wakati sisi hauyaoni hata kwa macho ni lazima sasa tuamke na tuweze kuyafanya madini haya yaweze kuwanufaisha watanzania wote’aliongeza Masanja.
Kutokana na hilo alisema mpaka sasa Serikali ina mikakati mbalimbali ya kuweza kuokoa shehena ya madini ambayo yanapotea na kisha kuwanufaisha baadhi ya mataifa kwa kuweza kudhibiti eneo la Mererani sehemu ambayo madini hayo yanatokea
Alidai kuwa mpaka sasa Serikali ipo kwenye mchakato maalumu wa kuweza kutoa ajira kwa walinzi ambao watalinda madini hayo na kisha ya kuyasindikiza sehemu yanapotakiwa ikiwa ni njia mojawapo ya kuweza kuokoa madini hayo yasiibiwe na kisha kwwenda kuuzwa nje ya nchi.
“tutaweka maaskari ambao wana mafunzo maalumu pale Mererani lakini pia hata lile eneo le Square Kilomita kumi nalo tutaweza kulizungushia uzio maalumu kwani tunaamini kuwa kwa kufanya hivyo tutaweza kuokoa madini hayo ambayo yana uza wa nje ya nchi na hayanufaishi Taifa lenyewe”alimalizia Masanja.
No comments:
Post a Comment