Wauza maji walioandamana wakificha nyuso zao kujikinga na mabomu ya kutoa machozi.
Polisi nchini Ivory Coast wame warushia mabomu ya kutoa machozi kwa waandamanaji,wanaoandamana katika mji wa kibiashara wa Abidjan, maandamano ambayo yameandaliwa na umoja wa wauza maji.
Mifuko midogo ya plastiki ya maji ya kunywa ambayo inanunuliwa Ivory Coast yote na hata Africa kwa ujumla.upigwaji marufuku maji hayo maarufu kama viroba kwa Tanzania, inasemekana ndio chanzo cha maandamano hayo, katazo ambalo lilitolewa mwezi uliopita,utasababisha wafanyabiashara wengi wenye kuuza maji, kukosa ajira na mahitaji muhimu.
Serikali ya nchi hiyo iliamua kupiga marufuku biashara hiyo ili kupambana na uchafuzi wa mazingira na kuupigia chapuo uchumi wa kijani.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment