Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 28 November 2014

WAKILI MKONO KALIPWA NA TANESCO SHS. 62.9 BILIONI

Nimrod Mkono 
Na Boniface Meena, Mwananchi
Dodoma. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema Kampuni ya Uwakili Mkono & Co. Advocates na Hunton & Williams ya Marekani imejiingizia Sh62.9 bilioni kwa ajili ya kuendesha kesi mbalimbali za Tanesco na IPTL hadi Septemba mwaka jana.
Profesa Muhongo aliyekuwa anatoa tamko la Serikali dhidi ya Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ya ufisadi wa Sh306 bilioni katika akaunti ya escrow, alilieleza Bunge jana kuwa licha ya gharama, mawakili hao bado wanaidai Tanesco Dola za Marekani 4.50 milioni (Sh7.8 bilioni).
“Kumalizika kwa mgogoro huu wa IPTL si tu kwamba kumetuondoa kwenye hatari ya kuendelea kukamuliwa na mawakili hawa, bali pia katika mazungumzo yaliyofanywa kati ya Tanesco na IPTL tumeweza kuokoa takriban Sh95 bilioni katika madai ya awali ya IPTL,” alisema.
Kama fedha za escrow ni za umma
Profesa Muhongo alisema madai ya PAC kwamba fedha zilizokuwa katika akaunti ya escrow zilikuwa za Serikali si ya kweli kwa kuwa si za umma, bali fedha zote ni za IPTL.
“Huu si ukweli zipo sababu kuu zinazothibitisha kuwa fedha hizo hazikuwa za Serikali,” alisema Profesa Muhongo.
Alisema fedha zote zilizokuwa kwenye akaunti ya escrow ni mali ya IPTL ambayo ikiwa wakala wa kodi inastahili kudaiwa na kulipa kodi yoyote ambayo haijalipa.
“Kwa msingi huo, taarifa ya PAC haisemi ukweli kuhusu fedha zilizowekwa katika akaunti ya escrow kuwa ni fedha za umma,” alisema Profesa Muhongo.
Alisema ili kuthibitisha kwamba fedha hizi siyo za umma, CAG katika ukaguzi wake wa hesabu za Tanesco wa Desemba 31, 2012, alielekeza kutoa fedha za escrow kwenye vitabu vya hesabu vya Tanesco na kupunguza deni kwa kiasi hicho.
“Tanesco ina madeni na haijawahi kutengeneza fedha za umma,” alisema.
Katika hatua nyingine, Profesa Muhongo alisema madai ya PAC kuwa hapakuwahi kuwa na kamati ya uendeshaji kwa kipindi chote cha mkataba wa PPA si ya kweli.
“Ukweli ni kwamba, kamati ya uendeshaji iliundwa kabla ya kuanza uzalishaji wa mtambo mwaka 2002 na imeendelea kuwapo hadi leo. Kamati hiyo ina wajumbe sita. Wajumbe watatu kati ya hao wanatoka Tanesco na watatu waliobakia wanatoka IPTL,” alisema Profesa Muhongo.
“Kwa msingi huo si kweli kwamba kamati ya uendeshaji haikuundwa kama ilivyoelezwa na Kamati ya PAC katika ukurasa wa 10.”
Hati za hisa za kampuni
Akijibu hoja ya PAC kwamba Wizara ya Nishati na Madini itambue usajili wa hati za hisa za kampuni, Profesa Muhongo alisema: “Tunaomba ieleweke kuwa siyo majukumu ya wizara kutambua na wala kujishughulisha na hati za hisa za kampuni binafsi.”
CREDIT: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment