Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya
Meneja Mauzo, wa StarTimes, David Kisaka (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu StarMedia kushusha bei ya ving'amuzi vyake msimu huu wa Sikukuu. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya .Startimes, Jack Yu
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Startimes, Jack Yu (kulia), akionesha moja ya siku za kisasa wanazoziuza msimu huu wa sikukuu.
Ofisa wa Kampuni ya StarTimes, Lan Chen. akiwa mbele ya simu za kisasa zinazouzwa wakati wa kipindi hiki cha kuelekea kwenye sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Taarifa kwa vyombo vya habari
StarMedia yashusha bei ya ving’amuzi vyake msimu huu wa sikukuu.
· Ni kutoka sh. 79,000/- mpaka 59,000/- ambapo endapo mteja akilipia kifurushi chochote na kufikia kiwango cha sh. 120,000/- atapatiwa simu ya bure aina ya S100 hii ni katika sharamshamra za msimu wa sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya.
Dar es Salaam, Novemba 26, 2014 … Katika kuhakikisha kila mtanzania anapata fursa ya kufurahia huduma ya matangazo ya digitali nchini kampuni ya StarMedia Tanzania wameamua kushusha bei ya ving’amuzi vyao vya StarTimes kutoka shilingi 79,000/- mpaka 59,000/- katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Mauzo wa kampuni hiyo, David Kisaka alibainisha kuwa bei hiyo iliyoshushwa ni kwa ving’amuzi vinavyotumia antena za nje na ndani au DTT na hii ni katika jitihada zetu kuhakikisha kila mtanzania anafikiwa na huduma zetu kwa gharama nafuu.
Kisaka amesema, “StarTimes tumedhamiria kuwahakikishia watanzania kuwa huduma zetu zitaendelea kuwa nafuu kulingana na hali halisi ya maisha tuliyonayo. Kulithibitisha hilo, ninayofuraha kubwa leo kuwatangazia bei mpya ya ving’amuzi vya antena za nje na ndani itakuwa ni shiling 59,000/- na sio shilingi 79,000/- kama ilivyokuwa awali. Bei hii mpya ni dhamira yetu ya dhati kabisa ya kuwapatia wateja matangazo ya digitali ya uhakika na kwa bei nafuu ambayo kila mtu ataimudu hata yule mwenye kipato cha chini kabisa.”
“Punguzo hili la bei linakwenda sambamba na ofa kabambe ambapo endapo mteja wa StarTimes atalipia kifurushi chochote kile na kunafikia kiwango cha shilingi 120, 000/- basi atapatiwa simu ya bure na ya kisasa kabisa aina ya S100 na hapa ninamaanisha kwa watumiaji wa ving’amuzi vya kawaida na madishi.
Kwa ving’amuzi vya kawaida inamaana akilipia kwa kiwango hicho ni sawa na kulipia kifurushi cha Mambo kwa mwaka mzima (10,000/-), Uhuru kwa miezi sita (20,000/-) na Kili kwa miezi minne (30,000/-). Na kwa upande wa madishi pia ni hivyo hivyo endapo akilipia vifurushi vya smart ambacho ni shilingi 32,000/- na special kwa shilingi 16,000/-,” aliendelea Bw. Kisaka.
“Mbali na ofa ya punguzo la bei na zawadi za simu pia mteja wa StarTimes akilipia kifurushi chochote kwa miezi mitatu atapatiwa ofa ya mwezi mmoja wa bure na atakayelipia mwezi mmoja na nusu au siku 45 atapatiwa nusu mwezi au siku 15 bure,” alisema na kuongezea Bw. Kisaka, “Lengo la kufanya hivi ni kuwafanya wateja wetu waendelee kufurahia zaidi chaneli na vipindi vyetu na pia kuwashawishi waendelee kulipia zaidi na chaneli zingine ili kupata uhondo zaidi kwani haitoshi tu kutazama chaneli na vipindi vya nyumbani.”
“Hivyo basi ningependa kuwasihi wateja wetu na watanzania kwa ujumla ambao mpaka sasa bado hawajaunganishwa na huduma za StarTimes basi wakati ndio huu kwani tumewashushia gharama za chini kabisa kwa lengo la kumfikia kila mtu. Ili kuweza kupatiwa huduma zetu basi ningewaomba mtembelee ofisi na maduka yetu, kwa sasa tunayo maduka sita jijini Dar es Salaam likiwemo hili la hapa mtaa wa Samora, Tegeta, Buguruni, Bamaga, Msimbazi-Kariakoo na Ukonga huku mengine kumi yakiwa mikoani zilizo huduma zetu.” Alimalizia Bw. Kisaka
Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa StarTimes Tanzania, Jack Yu alitumia fursa hiyo pia kuwapatia watanzania habari njema kuhusu simu mpya na za kisasa zitakazopatikana katika msimu huu.
“Kwa mara nyingine tena StarTimes tunawaletea simu za kisasa ambazo zitapatikana kwa bei nafuu kabisa katika maduka yetu ya Bamaga, Msimbazi na hili la Samora. Mbali na maduka hayo pia simu hizi zitapatikana kwenye maduka ya mawakala na washirika wetu kama vile Vodacom na Airtel.” Alisema Bw. Yu
“Simu hizi ambazo zitapatikana kwa bei nafuu ni zawadi yetu kwa wateja wetu na watanzania kwa ujumla watakaotembelea ofisi na maduka yetu. Aina ya simu ambazo zitakazopatikana ni P40 yenye garantii ya miezi 13, Planet 5 na Solar 5 ambayo mteja atapatiwa na power bank ya bure, zote hizi zitapatikana kwa bei ya shilingi 129,000/-, 225,000/- na 270,000/-”
“Simu hizi zina uwezo mkubwa wa kupata huduma zote ikiwemo kutumia laini mbili za simu, uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu (memory card ya GB 8 ya bure) kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya matukio mbalimbali, kamera ya mebele na nyuma kwa kupiga picha nzuri na za kuvutia, uwezo wa kupata intaneti yenye kasi (3G) itakayokuwezesha kuperuzi mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, Whatsap, Viber, Wechat na kadhalika. Ningependa kuchukua fursa hii kuwataka watu wajitokeze na kujinunulia simu hizi kwani ni chache.” Alihitimisha bosi huyo wa StarTimes.
No comments:
Post a Comment