Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 29 November 2014

CHINA YAFANYA SHEREHE YA MIAKA 50 YA UHUSIANO NA TANZANIA

 Mkuu wa Msafara wa Kikundi cha Sanaa cha Nanjing kutoka China akihutubia kwenye sherehe hizo.

 Balozi wa China nchini, Lu Youqing, akitoa hutuba 
katika hafla hiyo. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel
 Viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa China na Tanzania wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye sherehe hizo.
 Wasanii wa Kundi la Utamaduni la Nanjing kutoka China, wakionesha umahiri wa kucheza katika uzinduzi wa sherehe za kusherehekea miaka 50 ya Ushirikiano baina ya Watu wa Jamhuri wa China na Tanzania uliofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana usiku.

 Raia wa China na Tanzania wakiwa kwenye sherehe hizo wakiangalia onyesho lililokuwa likifanywa na kikundi cha Sanaa kutoka china cha Nanjing.
 Wasanii wa kikundi hicho wakionesha umahiri wa kucheza na nguo aina ya mitandio.
 Umati huu ukifuatilia onesho hilo.
 Maonesho mbalimbali yakiendelea.

 Msanii huyu akitumia kifaa  kiitwacho pina kutumbuiza. Anaweza kutumia kifaa hicho kutoa milio ya ainatofauti ikiwa ni pamoja na kukipuliza kwa kutumia pua yake.
 Msanii huyu (kuli) alionesha shoo ya kujibadilisha sura yake kwa sura tofauti zaidi ya sita. Jamaa ni noma huyo balaa. Hakika ilipendeza sanaaaaa
Kikundi cha Sanaa na Jeshi la Polisi kikitumbuiza katika sherehe hizo.


Na Dotto Mwaibale

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel amesifu uhusiano uliopo kati ya Tanzania na China.

Prof. Ole Gabrie alimwaga sifa hizo jana usiku katika onesho la utamaduni wa China lililofanyika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika tukio hilo lililokwenda sanjari na maadhimisho ya miaka 50 ya uhusiano wa nchi hizo mbili, alisema umezaa matunda ambayo yanaonekana hadi leo.

Alisema kuwa mataifa haya mawili yamekuwa yakishikamana, hivyo ni jukumu letu kuhakikisha uhusiano huo hautetereki.

Naibu katibu mkuu alisema kutokana na kushikamana kwa wananchi wake kuwe mfano mzuri kwa mataifa mengine ambayo yanaweza kuiga.

Alifafanua kuwa zipo faida nyingi za uhusiano huo ambazo ni kiuchumi kutokana na kupata misaada katika nyanja mbalimbali.

"Tukumbuke hata Rais wetu amekuwa akisaini mikataba ya miradi ya maendeleo kwa sababu tu tuna uhusianio mzuri na China.

"Pia kijamii tunaona sekta ya afya na elimu inapata mafanikio kutokana na misaada ambayo tunapata kutoka taifa hilo," alisema.

Alisisitiza kuwa tofauti za mataifa haya zisitugawe na kuwa hata wakati viongozi waasisi wa mataifa haya, Mwalimu Julius Nyerere na Mao Tse Tung walijenga urafiki bila kujali tofauti za umri.

"Hebu fikiria wakati huo Nyerere alikuwa na umri wa miaka 42 ama 43 hivi na Mao Tse Tung miaka 70 hivi lakini walijenga urafiki mkubwa ambao matunda yake tunayaona hadi leo," alisema.

Aidha, naibu katibu mkuu huyo alisifu namna inavyojali utamaduni na kusifu kikundi cha Nanjing kilichotumbuiza kwa kushirikiana na wasanii wa Tanzania ambapo kilionesha michezo mbalimbali kama sarakasi, uimbaji wa nyimbo, mazingaombwe michezo iliyowavutia watu wengi

Kikundi hicho cha Nanjing kimeweza kuonesha shoo zake zaidi ya nchi 50 duniani. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

No comments:

Post a Comment