Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 29 November 2014

LOWASSA AKANUSHA KUANZISHA MTANDAO AKAUNTI YA ESCROW

Mhe. Edward Lowassa

Mbunge wa Monduli, Edward  Lowassa, amelaani kikundi cha watu kilichoanzisha ukurasa wa mtandao wa Twitter kwa kutumia jina lake unaohusu suala la Akaunti ya Escrow.

 
Katika taarifa yake jana, Lowassa alisema kikundi hicho kimefungua mtandao huo kwa anuani ya Lowassa,@edwardlowasa.
"Toka bunge limeanza mjadala wa kadhia ya Escrow account, kuna mtu au kikundi kwa sababu wanazozijua wao wenyewe wameanzisha akaunti ya mtandao wa twitter kwa jina la Edward Ngoyai Lowassa," alisema katika taarifa yake.
 
Alisema kwa kutumia ukurasa huo, mtu huyo amekuwa akiandika masuala kadhaa kuhusiana na suala hilo la escrow account na kile kinachoendelea bungeni, ikionekana kama ni kauli ya Lowassa.
 
"Tunawaomba wananchi kupuuza yote yanayoandikwa katika ukurasa huo. Watanzania tuachane na tabia ya matumizi ya mitandao ya kijamii kupotosha umma, tutumie mitandao hiyo kwa kuhamasisha maendeleo, amani, umoja na mshikamano kwa taifa letu," ilisema taarifa hiyo.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment