Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 28 November 2014

NYALANDU APIGA MARUFUKU UCHIMBAJI NDANI YA HIFADHI

Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu.

Na Cynthia Mwilolezi, Arusha
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amepiga marufuku uendeshaji wa shughuli za uchimbaji madini ndani ya hifadhi za taifa nchini na kuagiza walinzi wa hifadhi hizo kukamata watu wote watakaoingia  ndani ya hifadhi hizo kwa shughuli hizo.


Aliyasema hayo jana  wakati alipokuwa kwenye  hifadhi ya Ziwa Manyara  akizindua vivutio viwili  vya utalii vya ujenzi wa njia ya kutembea kwa miguu ndani ya ziwa Manyara na eneo maalum la kuangalia viboko bila kuwa na mashaka ya usalama wa maisha ya watalii.

Nyalandu alisema kuwa hifadhi za wanyama ni maaluma kwa ajili ya hifadhi hizo tu na siyo kuzigeuza kuchimba madini kama ilivyo sasa na kusisitiza watu wote waliogeuza hifadhi kuwa migodi waondoke mara moja ndani ya hifadhi hizo.

“Naagiza kuanzia sasa watu wote walioingia ndani ya hifadhi zetu kuchimba madini waondoke mara moja na askari fanyeni kazi yenu, mkikuta mtu kamateni bila hata kumwonea aibu hata kama ni kiongozi,” alisisitiza.

Aidha alisema wapo baadhi wanaochimba madini hayo kw akigezo kuwa wana kibali, watu wote wakamatwe hata kama mtu ana kibali atolewe maana hifadhi ni hifadhi.

“Kwanza hifadhi zetu zote zina shehena ya madini, lakini kama tutazigeuza kuwa migodi tutaua utalii kwani wanyama watapotea, haiwezekani kabisa kuendesha shughuli mbili ndani ya hifadhi,” alisema.

 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment