Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 28 November 2014

PHILIP HUGHES AFARIKI KWA KUPIGWA NA MPIRA, PELE ANA NAFUU

Philip Hughes alifariki jana kwa kupigwa na mpira

Bendera zinapepea nusu mlingoti katika viwanja vya cricket nchini Australia katika kuomboleza kifo cha mcheza cricket Philip Hughes aliyefariki jana baada ya kupigwa na mpira. 

Salaam za rambi rambi zimeendelea kutolewa kutoka sehemu mbali mbali duniani. 
Baadhi ya wachezaji wa cricket wamekuwa wakiacha magongo ya mchezo huo milangoni mwa nyumba zao kama ishara ya kuomboleza kifo hicho.
Edson Arantes do Nascimento maarufu Pele
Naye mwanasoka wa maarufu wa zamani Edison Arantes do Nascimento almaarufu Pele amesema anaendelea vizuri baada ya kuwekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kutokana na kusumbuliwa na tatizo la njia ya mkojo.
Taarifa zinasema Pele alipelekwa hosptalini hapo na kuwekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Na kindumbwembwe cha ligi kuu ya England kinaendelea kesho ambapo Arsenal watasafiri kumenyana na West Bromwich Albion huku Manchester United wakipepetana na Hull City Mechi ambayo itatangazwa moja kwa moja na Idhaa ya Kiswahili ya BBC kuanzia majira ya saa kumi na moja kwa saa za Afrika Mashariki. 
Mechi nyingine Sunderland wataumana vikali na Chelsea na Liverpool wakikutana uso kwa uso na Stoke City.
..Ndondi za kulipwa za shirikisho la kimataifa, Aiba, zinaendelea wikendi hii nchini Argentina na Azerbaijan, huku klabu ya Twende ya Tanzania, ikizidi kupata kichapo kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika ya mchezo wa magongo mjini Bulawayo, Zimbabwe
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment