Waandishi wa habari wakipokea taarifa hiyo. (Picha habari na www.mwaibale.blogspot.com) |
Mwakilishi kutoka Kituo cha Usuluhishi (CRC), Elizabeth Muhangwa, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari. |
Viongozi wa Mashirika ya kutetea haki za binadamu wakipitia ripoti hiyo
Na Dotto Mwaibale
Utafiti uliofanywa na mashirika ya kutetea haki za binadamu katika utafiti wa awali kuptia mradi wa Gewe II kuhusu ukatili wa kijinsia hapa nchini umebaini waathirika wa matukio hayo hawana sehemu maalum ya kupeleka malalamiko yao.
Hayo yamesemwa Dar es Salaam leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Valeria Msoka, wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya utafiti wa awali za ukatili wa kijinsia.
Alisema utafiti huo umefanywa na Mashirika matano ya kutetea haki za Binadamu ambayo ni Chama cha Wanasheria wanawake (TAWLA), Chama cha Wanasheria wanawake Zanzibar (ZAFELA), Kituo cha Usuluhishi (CRC), Mtandao wa Jinsia
Tanzania (TGNP) na Chama cha waandishi Habari wanawake Tanzania (TAMWA)
Bara na Zanzibar.
Alisema utafiti huo umeonesha asiliamia 17 ya wananchi hawanauelewa wa sheria za ukatili hali inayopelekea kutokufuatilia haki zao wakati wa uvunjaji na wakati mwingine kutoripoti kabisa kesi hizo.
Alizitaja wilaya zilizofanyiwa utafiti huo kuwa ni Wete (Pemba kaskazini), Magharibi Unguja, Kusini Unguja (Kusini Unguja), Kisarawe (Pwani), Newala (Mtwara), Lindi Vijijini (Lindi), Mvomero (Morogoro) na wilaya mbili za Kinondoni na Ilala (Dar es Salaam).
Msoka aliitaja Lindi Vijijini kuwa ndio wilaya inayoongoza kuwa na uelewa mdogo wa asilimia 12 ambapo asilimia 21 ya uelewa kwa Wete Zanzibar kuwa ni mkubwa kuliko wilaya zote ulipofanyika utafiti huo.
"Ofisa mmoja wa Polisi Lindi alisema kesi nyingi huripotiwa katika hatua ya familia na hufikishwa mahakamani baada ya kushindwa kupata suluhu hivyo kuwa katika hatari ya kupata haki" alisema Msoka.
Aliongeza kuwa utafiti huo kwa ujumla uliona asilimia 47 za kesi huripotiwa katika Serikali za vijiji, asilimia 25 huripotiwa polisi nyingine huripotiwa Kamisheni ya Haki za Binadamu, Mashirika ya Hakli za Binadamu na kwa wanasheria wanaongoza (Para Legals).
"Hali hiyo ya kutokuwa na mfumo maalum wa kuripoti inaweka mazingira ya kutopatikana kwa haki na pia kukosekana kwa takwimu sahihi ya kesi za ukatili"
alisema Msoka.
Alisema taarifa hiyo inaonesha kuwa wananchi hawana majukwaa ya kukaa pamoja na kujadili changamoto zao ambapo ni asilimia 13.5 ndiyo wanachama wa vyama vya kijamii (Civil Society Associations).
Msoka
alisema kwa pamoja Mashirika hayo yanatekeleza mpango wa Usawa wa
Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake (GEWE) ambao unafanywa kwa mashirikiano
na Serikali ya Denmark.
No comments:
Post a Comment