Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday, 30 November 2014

ONGEZENI UZALENDO KUKUZA ELIMU - LAIZER


Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny BlogArusha: JAMII imeaswa kuhakikisha kuwa inaongeza kiasi kikubwa cha uzalendo hasa kwenye sekta ya elimu kwani kwa sasa wapo baadhi ya watu kwenye jamii ambao bado hawajajua madhara na faida za kupata au kukosa elimu.

Elimu ya sasa imepoteza sana Dira na haijengi uzalendo tofauti na miaka ya nyuma hali ambayo wakati mwingine inasababisha wengi wa wanafunzi kusoma ili kuonekana kama wamesoma na wala sio kwa ajili ya manufaa yao ya baadaye.
Changamoto hiyo imetolewa na Joseph Laizer ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya St Benedicto Meliyo iliyopo Sekei jijini hapa wakati akiongea katika kikao cha wazazi pamoja na walezi wa shule hiyo kilichofanyika mapema jana.
Lazier alifafanua kuwa neno uzalendo ni moja ya maneno ambayo yamesahulika sana hasa kwenye sekta elimu jambo ambalo wakati mwingine linawafanya wanafunzi wengi kujikuta wakiwa wanasoma kwa mazoea pekee.
Alidai kuwa kukosekana kwa uzalendo hasa kwenye sekta ya elimu ndio chanzo kikubwa sana cha elimu hapa nchini kushuka lakini kwa upande mwingine pia hata wahitimu katika ngazi mbalimbali za elimu nao kujikuta wakiwa wanahitimu wakiwa hawana maarifa yeyote ingawaje wamemaliza.
“Mwanafunzi anapopewa uzalendo naamaanisha kuwa anapewa mbinu, lakini hata maarifa mbalimbali ya kuweza kujifuza na kutumia vema elimu walizopewa lakini kwa sasa wengi wana wanafunzi wanajengewa maisha ya kwenda shule pekee na wala sio uzalendo wa kutumia elimu zao vema,” aliongeza hivyo.
Mbali na hayo ya uzalendo kwenye sekta elimu pia alidai kuwa ili Elimu hapa nchini ili iweze kusonga mbele kwanza kunahitajika mazingira mazuri pamoja na vifaa vya kutosha tofauti na sasa ambapo bado Serikali haijaweza kutimiza hayo yote hususani kwenye sekta binafsi za elimu.
Katika hatua nyingine alisema kuwa ili kuwa mfano bora wa shule ambazo zina uzalendo mzuri wa elimu wwameweka uataribu wa kutoa elimu kwa wazazi kwani hata wazazi wengine nao wamekuwa mwiba wa ukosefu wa uzalendo hasa kwenye elimu.
"Wakati mwingine wazazi wanakuwa mwiba wa elimu hasa pale wanapofikiria suala zima la ada pekee na kuacha kujua na kushirikiana na walimu juu ya elimu wanayoipata pindi wanapokuwa mashuleni sasa siyo hapa utaratibu ni kuwa kila mzazi atakuwa na elimu hiyo lakini hata suala zima la vipaji,malezi, makuzi, na hata maadili mema,” aliongeza Laizer.

No comments:

Post a Comment