Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 29 November 2014

BAN KI MOON ASTUSHWA PROFESA TIBAIJUKA KUHUSISHWA KASHFA YA ESCROW

Ban Ki Moon, Katibu Mkuu wa UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki Moon, ameshtushwa na tukio la Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Kazi, Profesa Anna Tibaijuka kuhusishwa wizi wa mabilioni ya shilingi unaosadikiwa kufanywa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.

 
Akizungumza juzi usiku nje ya ukumbi wa Bunge mjini hapa, Prof. Tibaijuka, pamoja na kuelezea madai hayo kuwa ni yenye lengo la kumchafua kisiasa, alisema amepokea pole nyingi kutoka kwa watu tofauti, akiwamo Ban -Ki-Moon.
 
Prof. Tibaijuka aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN-Habitat).
 
Tibaijuka alihusishwa na wizi wa Sh. bilioni 306 katika akaunti ya Escrow, kutokana na  kumbukumbu za Benki ya Mkombozi, kuonesha kuwa akaunti ya mmiliki wa asilimia 30 za Kampuni ya IPTL,  Rugemalila, kumpelekea Sh. Bilioni 1.6
Uchunguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ulibaini kuwa fedha hizo zilizopokelewa na Prof. Tibaijuka zilikuwa sehemu ya fedha ambazo Rugemalila, alilipwa na mmiliki wa kampuni ya Pan Afrian Power (PAP), ambaye chanzo chake cha fedha hiyo kilibainika kuwa ni akaunti ya Escrow.
 
"Mimi ningejuaje kuwa kaka yangu Rugemlila fedha alizotoa kuchangia maendeleo ya shule ninayodhamini, ameipata kutokana na mauzo ya hisa zake 30, katika kampuni ya IPTL?  Hapa ninachokiona, kama kuna kesi ya kujibu ni ya kubambikiwa kesi," alieleza Profesa Tibaijuka.
 
Alisema uchunguzi wa CAG haukumhusisha kwa namna yoyote na tukio la Akaunti ya Escrow, isipokuwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati ikishughulikia ripoti za CAG na Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
 
Alisema kamati hiyo ilimuingiza kwenye kashfa hiyo, kwa kilichoelezwa kuwa ni kufuatilia waliopata mgawo wa fedha zilizotokana na zile zilizochotwa kwenye Akaunti ya Escrow, ambazo kwa mujibu wa taarifa ya PAP haikuwa sahihi kulipwa ndiyo maana inaonekana kuwa imeibwa kwa kutumia ofisi na viongozi mbalimbali serikalini.
 
Alisema kuhusishwa na wizi huo ni wivu wa kisiasa na kwamba yeye ni miongoni mwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM). Aidha, jina la Profesa huyo ni miongoni mwa majina mbayo hivi karibuni, yalitawala anga za siasa nchini likitajwa kuwa miongoni mwa wanaoweza kupendekezwa kwenye uchaguzi mkuu mwakani, katika nafasi ya urais.
 
Alisema katika suala la maadili ya uongozi, yeye ni mbobezi na kwamba ndiyo maana alimudu kufanya kazi UN-Habitat, akisimamia miradi yenye thamani ya fedha nyingi bila kuguswa na kashfa ya aina yoyota na kuwa ndiyo maana hata Ban Ki Moon, alishtushwa na kuhusihwa kwake na kashfa ya Escrow.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment