Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Showing posts with label MATOKEO YA AJABU. Show all posts
Showing posts with label MATOKEO YA AJABU. Show all posts

Thursday, 24 October 2013

SIKU BOLI ZOZO ALIPOIBUKIA JANGWANI!

Kikosi cha Yanga cha mwaka 1994. Kutoka kushoto waliosimama ni Salum Kabunda 'Ninja', Constantine Kimanda, Steven Casmir Nemes, Kenneth Pius Mkapa, Selemani Mkati. Waliochuchumaa kutoka kushoto ni Nico Bambaga 'Machine', Sekilojo Chambua, Edibily Lunyamila, James Tungaraza 'Boli Zozo', na Said Mwamba 'Kizota'.

Na Daniel Mbega
YOUNG Africans, ambayo mwaka 1993 iliteswa sana na wapinzani wake wa jadi, Simba, baada ya kutamba misimu miwili ya nyuma, hatimaye Jumamosi Februari 26, 1994 iliingia kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwakabili ‘wanyama hao wakali’ wa Msimbazi, ambao mwaka huo walikuwa wameongeza makucha yao kwa kuwasajili wachezaji mahiri na wauaji wa mabingwa hao watetezi wa Tanzania Bara, Yanga.

Wednesday, 23 October 2013

MNALIKUMBUKA SCUD LA JANGWANI LILILOBOMOA MSIMBAZI MARA MBILI 1991?

Said Sued 'Scud' (wa tano kutoka kulia) akiwa na kikosi cha Yanga 1991


Na Daniel Mbega

ZIKIWA zimesalia siku tatu tu kabla ya pambano la Simba na Yanga, mashabiki wa timu hizo walikuwa wamepamba moto kucharurana mitaani, lakini wadadisi wa mambo walikuwa wamefikia uamuzi kwamba, pambano hilo lingekuwa kama fainali ya ligi hiyo, kwa sababu, timu yoyote ambayo ingeshinda Jumamosi Agosti 31, 1991 ingekuwa vigumu kuzuiwa na timu nyingine huko mbele isitwae ubingwa wa Tanzania Bara msimu huo.

Monday, 21 October 2013

YANGA FUNGA, SIMBA RUDISHA - KAMA 1996 VILE!

Picha kwa hisani ya jestina-george.com

SIMBA na Yanga zimetoka sare. Ni sare ambayo haikutegemewa na mashabiki wa Yanga waliokuwa wanaamini timu yao ingeweza kupata ushindi wa mabao mengi baada ya kuongoza kwa mabao 3-0 hadi timu zinakwenda mapumziko.

Sunday, 20 October 2013

DUA ALIVYOWADUWAZA YANGA 1993


 Dua Said

Na Daniel Mbega
LIGI Kuu ya Muungano iliyosadikiwa kuwa na msisimko wa kipekee msimu huo kwa vile ilikuwa inawahusisha kikamilifu mamilionea wote watano waliokuwa wanafadhili soka nchini Tanzania, ilianza rasmi Jumamosi Septemba 25, mwaka huo 1993 na ilitarajiwa kupamba moto zaidi Jumapili katika kindumbwendumbwe cha aina yake kwa kuzikutanisha Simba na Yanga.

SIMBA YANUSURIKA KUSHUKA DARAJA TENA 1988


Kikosi cha Simba cha enzi hizo.

Na Daniel Mbega
SIMBA, siyo tu kwamba iliokoka na kuteremka daraja msimu huo ukiwa ni msimu wa pili mfululizo kunusurika, bali ushindi wao wa magoli 2-1 dhidi ya mahasimu wao wakubwa, Yanga Jumamosi Julai 23, 1988 mwaka huo kwenye Uwanja wa Taifa uliifanya ilinde hadhi yake.

Saturday, 19 October 2013

JENERALI MKAMBI AFUTA UTEJA WA YANGA KWA SIMBA

 
Hamis Ramadhani Kinye alidaka mechi hiyo

Na Daniel Mbega
PENGINE msemo wa ‘Mvumilivu hula mbivu’ ndio ulioipa nguvu Yanga, kwani baada ya vipigo vya miaka mitatu mfululizo kutoka kwa Simba, hatimaye ilikata mzizi wa fitina na kuichapa goli 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa Septemba 5, 1981.
Inawezekana nao Simba walipitiwa na ule msemo ‘Ukiona Kobe kainama ujue anatunga sheria,’ ndiyo maana kila walipojaribu kuipenya ngome ya Yanga siku hiyo ilikuwa haipenyeki na hata walipofungwa goli hilo bado ‘waliamini’ wangesawazisha na kuongeza lingine kama ilivyokuwa kawaida yao. Juhudi zao zote zikawa kama zile za ‘mfa maji, ambaye haishi kutapatapa’.

Friday, 18 October 2013

YANGA YAGEUZWA NYANYA 1977

Kikosi cha Simba cha mwaka 1977 kilichopeleka maafa Jangwani.


 Na Daniel Mbega
KATIKA mchezo wa soka kushinda ama kushindwa ni mambo ya kawaida, lakini vipo vipigo ambavyo timu hupata kiasi cha kujiuliza mara kumi kumi, kulikoni? Kama kuna kipigo ambacho kitabaki katika kumbukumbu za Yanga milele na milele ni kile cha mwaka 1977 cha magoli 6-0 kutoka kwa watani wake wa jadi, Simba, kwenye mchezo wa Ligi ya Taifa.
Kwa waliokuwepo na waliopata simulizi baadaye, Jumanne ya Julai 19, 1977 ilikuwa siku yenye majonzi makubwa kwa mashabiki wa Yanga na furaha kubwa kwa wale wa Simba, ambayo kwa ushindi huo, mbali na kujihakikishia ubingwa wa Ligi ya Taifa kwa kuwa ilibakiza mechi moja tu dhidi ya Navy (sasa KMKM) ya Zanzibar iliyokuwa ya kukamilisha ratiba, pia ilikuwa imefanikiwa baada ya miaka tisa kulipa kisasi cha kufungwa magoli 5-0 na Yanga mwaka 1968.

UNAIKUMBUKA ‘THRILLER IN NYAMAGANA’ 1974?

Kipa wa Simba, Athumani Mambosasa, akiunyaka mpira huku akitazamwa na Kitwana Manara 'Popat' wa Yanga (kushoto).
Kikosi cha Yanga cha mwaka 1973 kabla Dk. Victor Stanculescu (wa pili kushoto) hajaondoka. Anayeongea na wachezaji na meneja wa timu, Shiraz Sharrif. Wengine ni Hassan Gobbos, Kitwana Manara, Maulid Dilunga, Sunday Manara, Elias Michael, Boi Idd 'Wickens', Selemani Said, Gibson Sembuli, Omar Kapera, Ally Yussuf, Abdulrahman Juma (nahodha).

Na Daniel Mbega

KWA wenye kumbukumbu nzuri bila shaka kipigo cha Nigeria cha magoli 2-1 toka kwa Italia katika raundi ya pili ya Kombe la Dunia huko Marekani mwaka 1994 kiliwarudisha mapema miaka ya 1970 pale Yanga ilipoichapa Simba magoli 2-1 kwenye fainali ya Ligi ya Taifa ya Soka kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza.

Thursday, 17 October 2013

SUNDERLAND YABUGIA 5-0 MWAKA 1968

Maulid Dilunga (kushoto) enzi ya uhai wake akiwa kamisaa wa mchezo wa soka. Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry.


Na Daniel Mbega
ILIKUWA jioni yenye majonzi na simanzi kupindukia kwa wachezaji, viongozi na wapenzi wa Sunderland Jumamosi ya Juni Mosi, 1968, kwani siyo tu siku hiyo walipata kipigo kisichovumilika cha magoli matano kwa gurudumu toka kwa Yanga, bali pia kipigo hicho kilitia saini Yanga kuchukua ubingwa wa soka nchini.

YANGA ILIPOCHAPWA 'FOUR-FOUR' MBELE YA KAWAWA


Mzee Hamisi Ally Kilomoni, mchezaji wa zamani wa Sunderland anayekumbukwa na Yanga kwa jinsi alivyokuwa anapachika mabao dhidi yao. Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry.
 
SUNDERLAND, ambayo wakati huo ilikuwa ikishikilia ubingwa wa kandanda wa Afrika Mashariki ‘Allsopps Cup’ pamoja na ubingwa wa Taifa, Jumapili ya Mei Mosi, 1966 iliinyoa Yanga bila maji kwa kuifunga magoli 4-0 katika Uwanja wa Ilala, mbele ya waheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais, Rashid Mfaume Kawawa, Mawaziri, Mabalozi, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Selemani Kitundu na maelfu ya watazamaji waliojazana hapo.

MABAO 156, MECHI 75 ZA SIMBA NA YANGA LIGI KUU

Furaha ya ubingwa kwa Simba 2012 huku wakisherehekea ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya mahasimu wao, Yanga.


Na Daniel Mbega
HUKU utasikia: “Simba! Simba! Simba!” halafu kule nako kutasikika: “CCM! CCM! CCM!” Naam, hivi ni vibwagizo vinavyosikika kila wakati Simba na Yanga zinapokutana, iwe kwenye mechi za Ligi, mashindano mbalimbali na hata zile za kirafiki.
Mashabiki wa Simba wanaweza kusikika pia wakisema: “Amesimama kidedea, eeee kidedea!” halafu upande mwingine utawasikia wakichombea: “Kitimtimu, mtakiona leo, nyumba ya shetani mwendawazimu kaingiaje!”

STARS ILIPOCHEZA KIFUA WAZI

 Rais wa Sudan, Jenerali Gaafar Mohamed el-Nimeiry akisalimiana na wachezaji wa Taifa Stars. Hapa anasalimiana na Hassan Gobbos 'Wa Morocco' na kushoto kabisa ni beki mstaarabu Mohammed Chuma. Anayemtambulisha kwa wenzake ni nahodha wa Stars Abdulrahman Juma. Mwingine pichani ni Kitwana Manara na anayeonekana uso wake ni Abdallah Kibadeni.

Na Daniel Mbega
KATIKA historia ya soka Tanzania kuna mambo ya kufurahisha kutokana na matoeo ya timu zetu uwanjani kama kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika 1980 na kuna mambo ya kusitikisha kama Simba kushindwa kutwaa Kombe la CAF mwaka 1993.
Hata hivyo, kuna mambo ya kufedhehesha ambayo hayasimuliki. Mambo haya, ni afadhali yatokee kwetu wenyewe, lakini yanapotokea mbele ya wageni aibu yake haifutiki kirahisi.

Tuesday, 15 October 2013

MAMBO KANGAJA HUENDA YAKAJA, YANGA FADHIL BWANGA....


Yanga Bwanga (kushoto). Picha kwa hisani ya zenjdar.co.uk


Na Daniel Mbega

NAMKUMBUKA mtangazaji nguli wa kipindi cha michezo cha Radio Tanzania Dar es Salaam (RTC wakati huo - sasa TBC Taifa), marehemu Abdul Masoud, katika siku ambayo Yanga ilimsajili kiungo mshambuliaji machachari Yanga Fadhil Bwanga kutoka kwa 'Wagosi wa Kaya' Coastal Union mwaka 1976 kama sikosei. Nilikuwa mdogo sana wakati huo, lakini ndiyo kwanza nilikuwa ninapenda michezo hasa tukiwa tunajikusanya nyumbani kwa Balozi wa Nyumba Kumi aliyekuwa na redio ya 'Mkulima' kila siku saa mbili kasorobo.