Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Showing posts with label BURUDANI. Show all posts
Showing posts with label BURUDANI. Show all posts

Monday, 30 January 2017

MLIMBWENDE WA SHINDANO LA MISS KIBOSHO 2017 JIJINI MWANZA APATIKANA.

Baada ya mtifuano mkali wa kumtafuta mlimbwende wa shindano la MISS KIBOSHO 2017 kufanyika kwa mara ya kwanza usiku wa ijumaa Januari 27, 2017 na jana jumamosi Januari 28,2017 katika Ukumbi wa Kibosho Luxury Bar Kiseke Ilemela Jijini Mwanza, hatimaye mshindi amejulikana.

Thursday, 26 January 2017

WASANII 400 WA AFRIKA KUTIKISA TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA ZANZIBAR 2017

Mkurugenzi wa tamasha la Sauti za Busara Bw.Yusuf Mahmoud akionesho moja ya kitabu chenye mambo lukuki yahuso tamasha hilo pamoja la habari mbalimbali za wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo la aina yake kwa wakazi wa Zanzibar na wageni waalikwa kutoka sehemu mbalimbali za nchi na nje.

Thursday, 19 January 2017

WIMBO MPYA WA ASILI WENYE VIONJO VYA KISASA KUTOKA KWA SEKO BWAY-NZUGWI

Pata fursa ya kusikiliza wimbo mpya wa asili ya kisukuma kutoka kwa mwanamuziki Seko Bway. Wimbo unaitwa Nzugwi na umeimbwa kwa vionjo vya muziki wa kisasa. Umetengenezwa na King Fenya kutoka Mbunda Records ya Jijini Mwanza.
Bonyeza hapa kusikiliza

Monday, 16 January 2017

VIDEO: BINTI ALIYE MDATISHA MWANAUME MTANDAONI KWA PICHA ZISIZO ZAKE AAIBISHWA

Ni jambo la kusisimua kutokana na huruka za vijana kwenye mitandao ya kijamii, hii ni mara baada ya kuona matumizi mabaya ya mitandao kama Facebook,Twitter, Instagram nk vikiongezeka. Vijana wengi  wanashindwa kutumia mitandao ya kijamii  kwa ajili ya masilahi yao badala yake wamekuwa wakitumia mitandao hiyo, kutafuta wapenzi,utapeli, umbeya, kuanika nyeti zao yaani kuweka picha chafu nk.

Monday, 9 January 2017

SERA YA FILAMU KUWAKOMBOA WASANII TANZANIA

Katibu Mtendaji, Bodi ya Filamu nchini Tanzania, Mama Joyce Fissoo.


Na BMGHabari
Bodi ya Filamu nchini imebainisha kwamba kukamilika kwa sera ya kusimamia uendeshaji wa tasnia ya filamu, kutasaidia kuwakomboa wanatasnia hiyo kwa kuinua kuinua uchumi wao na wa Taifa kwa ujumla.

Saturday, 7 January 2017

BODI YA FILAMU NCHINI YAWAOMBA WATANZANIA KUZIPIGIA KURA FILAMU ZA KITANZANIA KWENYE TUZO ZA AMVA 2017

BMGHabari
Bodi ya Filamu nchini imewahamasisha watanzania kuongera ari ya kuzipigia kura filamu za kitanzania zinazowania tuzo za Africa Magic Viewers Awards (AMVA 2017) za nchini Nigeria.

Friday, 23 December 2016

BASATA YAPIGA MARUFUKU DISKO TOTO


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini linawakumbusha wamiliki na waendeshaji wa kumbi za burudani kufuata sheria, kanuni na taratibu walizopewa kwenye vibali vyao vya uendeshaji wa kumbi.

Friday, 16 December 2016

KATIBU TAWALA MKOANI MARA AHITIMISHA MAFUNZO KWA WADAU WA FILAMU MKOANI HUMO.

Katibu Tawala mkoa wa Mara, Adoh Mapunda (katikati) akizungumza hii leo kwenye kilele cha mafunzo ya siku tatu kwa wadau wa filamu mkoani humo. Mafunzo hayo yalianza juzi Disemba 14,2016 kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Mara Mjini Msoma.

Thursday, 15 December 2016

ZAIDI YA WANATASNIA 200 WA FILAMU WANUFAIKA NA MAFUNZO MAALUMU YA FILAMU MKOANI MARA.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nuru Milao (kulia), akifungua warsha (mafunzo) ya siku tatu kwa wanatasnia ya Filamu na Maigizo mkoani Mara, yaliyoanza hii leo katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Mara iliyopo Musoma Mjini. Wengine ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fisso(katikati) pamoja na Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba (kushoto).

BODI YA FILAMU NCHINI YAENDELEA KUWANOA WANATASNIA WA FILAMU MKOANI MARA.

Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, akiongozana na Naibu Katibu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Milla pamoja na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fisso, kwenye ufunguzi wa Mafunzo ya siku tatu kwa Wanatasnia wa Filamu na michezo ya kuigiza mkoani Mara, yaliyoanza jana kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Mara Mjini Musoma.

BODI YA FILAMU NCHINI YAWATAKA WADAU KUFIKISHA MISWADA YA FILAMU KUKAGULIWA KABLA YA KUIGIZWA.

Bi. Deograsia Ndunguru ambaye ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Sanaa na Habari, Chuo Kikuu Dodoma UDOM, hii leo akiwasilisha mada kwenye mafunzo ya siku tatu kwa wanatasnia wa filamu na maigizo mkoani Mara, yaliyoanza jana ukumbi wa shule ya Sekondari Mara. Mafunzo hayo yameandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Bodi ya Filamu nchini.
#BMGHabari

Tuesday, 13 December 2016

FURAHIA WIMBO MPA WA MSANII CASTLE MC-NIMERUDI.

Castle MC ni msanii chipukizi kutoka Jijini Mwanza. Ameachia wimbo mpa uitwao "Nimerudia" akimshirikisha H.Criss. Wimbo umetengenezwa na producer Day Dream kutoka studio za Over The Classic Music Jijini Mwanza.

Wimbo unavutia kusikiliza na unatoa ujumbe wa watu wengi walio kwene mahusiano ambapo baada ya kutengana, mmoja hurudi na kutaka kufufua upya mahusiano.
Hakika ni HipHop ya maana kusikiliza.
Bonyeza HAPA Au Play Hapo Chini

Saturday, 3 December 2016

MREMBO ANNA NITWA AFANIKISHA UKARABATI WA CHOO CHA WODI YA KINAMAMA WANAJIFUNGUA WATOTO NJITI HOSPITALI YA DODOMA

 Mlimbwende anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma 2016/17), Anna Nitwa (wa pili kulia) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (wa pili kushoto) pamoja na madaktari wakati wakielekea kwenye Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Desemba 1, 2016.

KAMA MSANII UNATAKA KUJUA HAKI ZA KAZI ZAKO ZA SANAA.., BASI JUKWAA HILI SIO LA KUKOSA!


Wednesday, 23 November 2016

WAREMBO WA MISS UNIVERSE TANZANIA 2016 WAANZA KAMBI

Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications L.T.D,Maria Sarungi Tsehai (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,kuhusu kuanza kambi kwa warembo wa Miss Universe Tanzania 2016 ambapo fainali itafanyika Novemba 25 katika Hoteli ya Collessium iliyopo Oysterbay. Kulia ni Mkurugenzi wa Hoteli ya Collessium,Mustafa Dhanji na Mratibu wa shindano hilo,Mwanakombo Salim.(PICHA NA ELISA SHUNDA)

Sunday, 20 November 2016

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA ZIFF AZINDUA TAMASHA LA UONESHAJI FILAMU BURE MKOANI GEITA

Waziri wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith Kombo, akizungumza kwenye Uzinduzi wa Tamasha la Uoneshaji wa Filamu kwa njia ya Sinema mkoani Geita, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Nape Nhauye.

WANATASNIA YA FILAMU MKOANI GEITA WAPEWA MTIHANI WA KUANDAA TAMASHA LA FILAMU

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fesso (kushoto), akizungumza kwenye kikao cha Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita hii leo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Geita. Mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye, aliyewakilishwa na Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Mahmood Thabith Kombo (wa pili kushoto). Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti Chama cha Waigizaji mkoani Geita, Rosemary Michael na anayefuata ni Herman Matemu ambaye ni Kaimu Afisa Tawala mkoa wa Geita.

Thursday, 17 November 2016

SEMINA YA MUONGOZO KWA WASANII WALIOTEULIWA TUNZO ZA EATV YAFANYIKA DAR

Mratibu wa tuzo za EATV toka Baraza la Sanaa la Taifa Seleman Mabiso akifafanua jambo mbele ya wasanii walioteuliwa kuwania tunzo hizo.

Saturday, 12 November 2016

MKUU WA WILAYA YA NYAMAGANA ATOA SIKU SABA UTEKELEZAJI WA MAADHIMIO YA WASANII WA FILAMU

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Mary Tesha (kushoto), akipokea cheti cha utambuzi kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fesso (kulia), wakati wa ufungaji wa Mafunzo kwa Wasanii wa Filamu mkoani Mwanza yaliyoanza juzi Novemba 10 na kutamatika leo Novemba 12,2016 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Mhe. Tesha amemwakilisha mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella. Na BMG

BODI YA FILAMU NCHINI YAWATOA GIZANI ZAIDI YA WASANII 300 WA FILAMU MKOANI MWANZA

Zaidi ya wasanii 300 wa filamu mkoani Mwanza, jana wakifuatilia mafunzo kuhusu weledi wa sanaa ya filamu kutoka kwa mkufunzi, Richard Ndunguru, wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam.