Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 5 June 2014

HUYU NDIYE SUPER MOGUL DAVIS MOSHA MTANZANIA WA KWANZA KUMILIKI GARI LA AJABU HAPA BONGO ONA HAPA MWENYEWE LIVE!!

Gari la aina ya Lamboghirn gharama yake kwa hela za Tanzania ni Shillingi Billioni Moja na Nusu (1,500,000,000). Davis anakuwa Mtanzania wa kwanza kumiliki gari hili la kifahari ambalo ili ulinunue ni lazima uende kiwandani na kutoa order maalum tu na sio vinginevyo. 
Hata huko USA Star Mweusi wa kwanza na wa mwisho kulimiliki alikuwa ni Mike Tsyon miaka kama 15 iliyopita, lakini vinginevyo wengine wote wamekuwa wakiendesha kwa kukodi tu kutoka kiwandani na sio kulimiliki.
Mwaka 1992 Mike Tyson alilinunua kwa USD $ 400,000. 
Davis ambaye ameoa na ana watoto watatu ni mmoja wa mfano mkubwa sana wa kuigwa kwa wengine kwamba kazi ngumu na nidhamu pamoja na uvumilivu mwisho hulipa na kwamba hakuna njia ya mkato kwenye maisha, na ikipatikana kwa mkato itaishia kwa mkato huo huo.
Davis amewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga na kuipatia mafanikio makubwa.

No comments:

Post a Comment