Uchaguzi nchini Libya
Upigaji kura umeanza nchini Libya ambapo raia wanachagua bunge jipya.
Bunge hilo litachukua nafasi ya baraza la kitaifa ambalo limekuwa likikumbwa na migawanyiko ya kisiasa na kimawazo kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Wananchi wa Libya wanaendelea kupiga kura kuchagua wabunge wapya.Huu ni uchaguzi wa pili kufanyika nchini humo tangu kumalizika kwa mapigano yaliyomng'oa mamlakani aliyekuwa kiongozi wa mda mrefu Muamar Ghaddafi .
Wanatumaini kuwa huu utakua mwanzo mpya baada ya malumbano ya kisiasa yaliyoshuhudiwa tangu kuchaguliwa kwa bunge la kwanza mwaka 2012.
Inaelekea kuwa idadi ya wapigaji kura ni ndogo ikilinganishwa na idadi ya wapigaji kura waliosajiliwa.
Wagombea wapatao 2000 wanagombea nafasi 200 za ubunge.
Kutokana na hofu ya usalama idadi ya waangalizi wa kimataifa ni chache.
Eneo la mashariki la Libya limekuwa likikabiliwa na machafuko yanayoshukiwa kuchochewa na makundi ya wanamgambo.
Maafisa wa uchaguzi wanatarajia shuguli za upigaji kura kutatizwa katika baadhi ya miji.
BBC
No comments:
Post a Comment