TAARIFA KWA UMMA
KUHUSU WAJUMBE WA BARAZA KUU NA MKUTANO MKUU WA CHADEMA KWENDA KWA MSAJIRI WA VYAMA VYA SIASA NA KWA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI.
A.UTANGULIZI
Ndugu wanaHabari,
Mtakumbuka kwamba Juzi, katibu wa CHADEMA mkoa wa Tabora kwa niaba yetu wajumbe 78 wa baraza kuu na viongozi wengine wa mabaraza ya vijana na wanawake 4 kufanya kuwa jumla ya wajumbe 82 kwa pamoja tulizungumza na waandishi wa habari kuzungumzia maswala mbali mbali yanayotishia ustawi wa chama chetu.
Na mtakumbuka kwamba tuliazimia kwamba tutakwenda kumuona msajiri wa vyama vya siasa ili tumpatiemalalamiko yetu haya.
B. KWENDA KWA MSAJIRI WA VYAMA VYA SIASA.
Ndugu wanaHabari, Mapema leo Tumekwenda ofisini kwa msajiri wa vyama vya siasa na
tumekabidhi
barua yenye malalaiko mbali mbali juu ya uvunjifu ya KATIBA unaofanywa
kihuni na kwa makusudi na viongozi wetu wa CHADEMA hasa mwenyekiti Mbowe
na Katibu mkuu SLAA. Tunaambatanisha na nakala ya barua tuliyoipeleka
kwa msajiri.
C. KWENDA KWA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI.
Ndugu
wanaHabari, Kutokana na Ukweli kwamba viongozi wetu hasa Mwenyekiti
Mbowe na Katibu Mkuu SAA, wanahusika moja kwa moja na Ubadhirifu wa
fedha za chama zinazotokana na kodi za Umma, za zaidi ya BILIONI 10.038
na wao wanasema hayo madai siyo mapya na kwamba wameyazoea.
Hivyo
basi tumepeleka kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali,
barua yenye kuomba kupatiwa nakala ya Taarifa ya Ukaguzi wa hesabu za
CHADEMA baada ya ofisi yake kukamilisha ukaguzi huo.
Pia
pamoja na kuomba Nakala hiyo, tumeomba pia mkaguzi azitoe taarifa hizo
hadharani ili wanachama wa CHADEMA na watanzania kwa ujumla waone
kilichopo ndani yake.
D. MSINGI WA HOJA ZETU.
Tunamuomba katibu mkuu wa chama, ajibu hoja zetu na aache kuleta viroja kama ambavyo amenukuliwa na vyombo vya hbari jana.
Msingi
wa hoja zetu sisi ni katibu mkuu kujilip zaidi ya million 130 kwa mwaka
huku makatibu wake wa mikoa, wilaya na kata wakilipwa shilingi 0.
Msingi
wa hoja zetu ni katibu mkuu SLAA kujikopesha zaidi ya Millioni 160
kwenda kumalizia deni la nyumba yake bila kufuata utaratibu wowote wa
kukopa.
Msingi
wa hoja zetu ni kitendo cha mbowe kutukodishia magari yake kwa
mamillioni ya pesa kila tunapotumia, halafu yanapokuwa chakavu anatuuzia
FUSSO MBILI chakavu kwa million 600.
Msingi
wa hoja zetu ni kitendo cha MBOWE kukiuzia chama VX V8 MBILI ambazo
amenunua kwa pesa za chama halafu anazisajiri kwa jina la MBOWE HOTELS.
Hiyo
ndio misingi ya hoja zetu, Slaa alitakiwa kujibu hoja hoja hizi, aeleze
ni kwanini anatumia vibaya pesa za umma hata kabla hajaingia
madarakani, SLAA aeleze kama leo tupo wapinzani tunachezea katiba hivi,
je tukiingia madarakani tutakuwaje?
SLAA
aeleze kama sisi viongozi wake wa wilaya ni WAJINGA, nay eye ndio
katibu mkuu wetu, sasa je yeye ni KUBWA JINGA?, AU MJINGA MKUU?, AU
ZEZETA? Unawezaje kukaa na viongozi WAJINGA, ukawaomba ushauri,
ukawatumia halafu wakikusoa ndio ukawajua kuwa WAJINGA, je SLAA sio
MJINGA ZAIDI YETU?
E. KUHUSU KUWAKANA WAJUMBE NA WANACHADEMA.
Ni
vema mkatambua kuwa viongozi wakuu wa CHADEMA wanakimbilia Kuwakana
wanachama na viongozi wake pindi linapotokea swala bila kujibu vilivyopo
ndani ya swala hilo, jana wamemkana JOSEPH YONAH ambaye ni mwenyekiti
halali wa CHADEMA wilaya ya temeke kiasi cha mwanzoni mwa mwaka huu
KUMTEKA NA KUMTESA.
Lakini pia huu hapa ni mwendelezo wa tabia ya CHADEMA KUWAKANA VIONGOZI WAO NA MATENDO YAO.
· Alipouwawa
CHACHA WANGWE, na ilipotangazwa kwamba wakati anauwawa alikuwa na ndugu
DEUS MALLYA ambaye ni mwanaChama wa CHADEMA kwenye Gari, asubuhi yake,
Ndugu John Mnyika, alimkana na kusema hamtambui na kwamba serikali iseme
DEUS MALLYA NI NANI na anatokea wapi?, na mambo mengineyo, na DEUS
MALLYA naye akajidai hamjui, alipotoka GEREZANI akamuomba msamaha kwa
kumkana.
· Alipojihudhuru
uenyekiti wa Mkoa wa SINGIDA muasisi wa CHADEMA mkoani Humo, ndugu
Wilfred Kitundu, Chadema badala ya kujibu hoja zake Walimkana
· Alipojiondoa
chamani katibu wa sekretariety na muajiriwa wa chama ambaye pia ni
mwenyekiti wa mkoa wa Lindi, ndugu Ally Chitanda, chadema hakujibu hoja
zake wakamkana
· Mzee
EDWIN MTEI alipotoa kauli kwamba TUME YA MABADILIKO YA KATIBA ni ya
KIDINI na kwamba KIKWETE ameteua WAISLAM WENGI kuliko wakristo, MBOWE
AKAMKANA
· JOSHUA
NASSARY alopotoa kauli kwamba mikoa ya KASKAZINI itajitenga na
kuanzisha nchi yao ya JAMUHURI YA KASKAZINI, Mbowe akamkana.
· Hata
MBOWE mwenyewe alipotangaza Hadharani kwamba amerudisha gari la
kiongozi wa UPINZANI BUNGENI na kwamba halitaki tena, AKAJIKANA na
AKAENDELEA KULITUMIA MPAKA LEO
· Hata MNYIKA na LISSU na wabunge wengine walipotangaza kutokuchukua POSHO BUNGENI, WALIJIKANA NA WANAENDELEA KUCHUKUA MPAKA SASA
· Hata
MBOWE na SLAA walipotangaza kwamba CUF ni CCM B na MBATIA ni kibaraka
wa CCM WAKAJIKANA na leo Wamejiingiza humo humo na kuungana nao
Hivyo tunawataka wawe na hulka za kujibu hoja na sio kukimbilia kuwakana watu ambao ni wanachama halali.
Sasa kama kilan atakayekosoa anakanwa, nani atabaki?, nani mwanachama halali, MBOWE na SLAA TU ama?
Tamko hili limesomwa leo 25.6.2014 na;-
JORUM ABDALLAH MBOGO
………………………………………..
MWANACHAMA WA CHADEMA
MWENYEKITI WA CHA CHADEMA WILAYA YA KALIUA
MJUMBE WA BARAZA KUU LA CHADEMA TAIFA
MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CHADEMA TAIFA.
Tunaambatanisha na nakala za Barua za kwa Msajiri na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu.
MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI
MTAA WA SAMORA NA OHIO
S.L.P 9080
DAR ES SALAAM
DAR ES SALAAM.
Ndugu.
YAH: MAOMBI YA TAARIFA YA UKAGUZI WA CHADEMA.
Husika na somo hapo juu.
Mimi
ni mwanachama na kiongozi wa ngazi ya wilaya wa Chama cha Demokrasia na
maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la chama
Kwa
kipindi kirefu ndani ya chama chetu tumekuwa tukilalamikia matumizi
mabaya ya pesa hasa za ruzuku, pesa ambazo msingi wake ni kodi za
wananchi na hivyo kuwa ni pesa za umma. Hii inatokana na ukweli kwamba
mpaka sasa chama kimepokea jumla ya BILION 10.038 kama ruzuku kutoka serikali kuu, kwa kipindi cha miezi 42 kutokea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010
Tumejitahidi sana kudai taarifa sahihi za matumizi ya pesa hizo bila mafanikio.
Kwa kuwa tunatambua kwamba ni hivi karibuni tu, ofisi yako imemaliza kufanya UKAGUZI MAALUM WA MAHESABU KWA VYAMA VYA SIASA kikiwemo na CHADEMA, na kwamba taarifa yake mmeshaiwasilisha Bungeni.
Kutokana na ukweli kwamba wengi wetu sisi sio wabunge na hatuna uwezo wa kuipata hiyo Taarifa ambayo ni muhimu sana.
Na
kwa kuzingatia kwamba sisi ndio wenye chama na sisi ndio walipa kodi
zinazoipatia chama Ruzuku. Ni wajibu wetu kusimamia matumizi yake.
Hivyo basi, kwa niaba ya viongozi na wanachama wenzangu wasiopungua 82, tunaiomba ofisi yako itusaidie yafuatayo
1. ITUPATIE NAKALA YA TAARIFA ILIYOKAGULIWA
2. IITOE NAKALA HIYO KWA UMMA ILI UMMA UJUE NAMNA KODI ZAO ZINAVYOTUMIWA
Tunatumaini kwamba Ombi letu litashuhulikiwa kwa uzito na umuhimu wa kipekee
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati.
Wako katika ujenzi wa Taifa
……………………………………………………
JORUM ABDALLAH MBOGO
MWANACHAMA WA CHADEMA
MWENYEKITI WA CHA CHADEMA WILAYA YA KALIUA
MJUMBE WA BARAZA KUU LA CHADEMA TAIFA
MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CHADEMA TAIFA.
Nakala :- Vyombo vya habari
MSAJIRI WA VYAMA VYA SIASA
S.L.P 63010
DAR ES SALAAM
TANZANIA
Ndugu,
YAH: MAOMBI YA UFAFANUZI WA KIKATIBA JUU YA UVUNJIFU WA KATIBA NA YA CHAMA UNAOFANYWA NA VIONGOZI
Mheshimwa Msajiri, Somo hapo juu la husika.
Mimi ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,
Kwa
niaba ya wanachama wenzangu, tunaleta kwako malalamiko ya uvunjifu
wa katiba ya chama Yanayotokana na matamko yanayoendelea kutolewa na
viongozi wa kitaifa juu ya kuungana na UKAWA yenye tafsiri kwamba
wataachiana majimbo ya kugombea ili waweze kuingia madarakani na kuunda
serikali ya pamoja.
kama hivyo ndivyo wanakiuka SURA YA TISA. IBARA YA 9.3.1 ya KATIBA YA CHADEMA inayosema ‘’chama
kinaweza kuunda mseto na chama au vyama vingine vyenye madhumuni na
malengo yanayofannaili kuimarisha iwezo wa kushinda uchaguzi mkuu au wa
serikali moja ya mtaa kwa lengo la kuunda utawala wa pamoja’’
Kwa
kuwa viongozi wa CHADEMA na CUF na NCCR wameungana na kuunda chama
kingine cha UKAWA kwa mujibu wa SURA YA TISA ibara ya 9.3.3 ‘’chama kinaweza kuungana na chama ama vyama vingine kuunda chama kipya’’ hivyo wamevunja SURA TISA, Ibara ya 9.3.4 inayosema ‘’Uamuzi kuhusu vipengere 9.3.1, na 9.3.3 utafanywa na mkutano mkuu wa Taifa na kuhusu kipengere 9.3.2 na Baraza KUU’’.
Na
hivyo sisi kama chama hatujakaa BARAZA KUU ili kupitisha AGENDA za huo
mkutano mkuu na wala MKUTANO mkuu haujaitishwa kujadili maamuzi hayo
yaliyofikiwa na viongozi wetu.
Mheshimiwa
Msajiri, Tunafahamu kwamba KANUNI za chama SURA YA TISA kuanzia ibara
ya 9.0 Mpaka ibara ya 9.7 zinatoa uhuru wa chama kuungana na kufanya
ushirika na vyama vingine kwa kadri itakavyoona inafaa.
Ila kanuni hizi zinaweka mkanganyiko wa kitafsiri, na hivyo zinazuiwa na kuuliwa nguvu na Ibara ya 9.2.3 yaKATIBA YA CHAMA Inayosema ‘’kukitokea migongano kati ya kipengele cha katiba na kile cha kanuni, kipengele cha katiba kitatawala’’. Hivyo kanuni zinazotoa uhuru huo haziwezi kutumika hapa.
Mheshimiwa
msajiri, kwa kuwa wewe ndio mlezi na msimamizi wa vyama vyote vya
siasa, na kwa kuwa hakuna chama cha siasa kilicho juu ya katiba yake,
hivyo tunakuomba uingilie kati mgogoro huu wa uvunjifu wa katiba
unaofanywa kwa makusudi na viongozi wa chama.
Tunakuomba
pia uuagize uongozi wa kitaifa uitishe haraka kikao cha baraza kuu,
kwani tumeshapitisha miezi mi nne sasa ya kisheria ambayo baraza kuu
lilipaswa kukaliwa, mara ya mwisho tulikaa kikao cha baraza kuu mwezi
febryary mwaka 2013, hivyo tulitakiwa tena tukae baraza kuu mwezi
February mwaka huu. Hatujaitwa, wala hatujapewa sababu yoyote yenye
mantiki.
Vile
vile tunakuomba uwaagize viongozi wa chama waitishe chaguzi halali za
zhama na waache kuchomeka watu wao wanaowataka kwa hila, kwa mujibu wa
ratiba tulizozipitisha uchaguzi ulupiswa kuwa umeshafanyika kufikia
December 2013, na baadae june 2014, lakini mpaka tunavyokuandikia leo,
hakuna lililofanyika.
Tunakutakia kila la heri katika kutusaidia ufafanuzi huu.
Tunatanguliza shukrani za dhati na tukiamini swala letu litafanyiwa linavyostahili.
Wako katika ujenzi wa Taifa.
JORUM ABDALLAH MBOGO
………………………………………..
MWANACHAMA WA CHADEMA
MWENYEKITI WA CHA CHADEMA WILAYA YA KALIUA
MJUMBE WA BARAZA KUU LA CHADEMA TAIFA
MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CHADEMA TAIFA.
Nakala :- Vyombo vya habari
No comments:
Post a Comment