Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 25 June 2014

AJIRA MPYA ZA WALIMU HIZI HAPA


TANGAZO 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

Utangulizi:
Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI imewapangia vituo vya kazi ya ualimu walimu waliohitimu Vyuo vya Ualimu Mwaka 2013 kuchukua nafasi za walimu ambao hawakuripoti katika vituo walivyopangiwa kwa ajira ya Machi 2014.
Baadhi ya waombaji hawakupangiwa vituo vya kazi kutokana na kutokuwa na sifa zinazostahili kuajiriwa katika utumishi wa umma kwa mfano:- umri na maombi kutoambatanishwa na

vithibitisho muhimu n.k.
Maelekezo kwa Walimu Ajira Mpya
  1. Kuripoti kwa Wakurugenzi wa Halmashauri walizopangiwa kwa ajili ya kupangiwa vituo kuanzia tarehe 25/6/2014, hadi tarehe 30/6/2014.
  2. Mwalimu ambaye hataripoti ifikapo tarehe 30/6/2014 hatapokelewa tena na nafasi yake atakuwa ameipoteza.
  3. Walimu hawa ni wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi kufuatia Orodha iliyotangazwa Machi 2014 hivyo OWM – TAMISEMI haitafanya mabadiliko yeyote ya vituo katika orodha hii.

Imetolewa na: -
OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI
ZA MITAA.

Juni 23, 2014: AJIRA KWA WALIMU WAPYA NA VITUO WALIVYOPANGIWA

  1. Walimu wa Astashahada (bofya hapa)
  2. Walimu wa Stashahada (bofya hapa)
  3. Walimu wa Shahada (bofya hapa)

No comments:

Post a Comment