Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 26 June 2014

SIKIA UNYAMA HUU: BAADA YA MTOTO NASRA, BABA AMFUNGIA MWANAWE NDANI KWA MIEZI SABA, HAKUNA KWEND AHAJA CHOONI!


Mtoto Erick ameadhibiwa kwa kujisaidia ndani badala ya kwenda chooni

Polisi katika wilaya ya Bukoba nchini Tanzania imemkamata baba wa mtoto kwa tuhuma za kumfungia na kumwadhibu mwanawe wenye umri wa miaka sita kwa muda wa miezi saba ndani bila kutoka nje.
Mtoto huyo ameyapata masaibu hayo kwa madai kwamba haendi haja chooni.Kwa mujibu wa afisa mtendaji wa eneo hilo, mtoto huyo ana makovu ya kupigwa mwili mzima ambayo hata baada ya miezi sita hayawezi kufutika.
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Bwizanduru, Edward Muhezi anasema Emmanuel Justinian aliamua kumfungia ndani mwanawe Erick Emmanuel kwa muda wa miezi saba bila kuona jua huku akimcharaza viboko.
Alifungiwa ndani na kuadhibiwa kwa muda wa miezi saba.

Inaidaiwa kwamba kushindwa kwa mtoto huyo kutojisaidia chooni kulimkera babake na hatimae aliamua kumfungia kwa muda wote huo na kumcharaza viboko ambayo inasemekana vimemsababishia maumivu makali Erick.
"Mtoto amezidiwa sana na ana majeraha makali, bado yupo hospitalini na tunasubiri ripoti ya madaktari," alisema Edward Muhezi.
Awali afisa huyo alielezewa kwamba mtoto huyo anasoma, lakini baada ya uchunguzi na kuwasiliana na majirani katika eneo hilo, anasema waligundua kwamba mtoto huyo amekuwa akiteswa.
Kwa mujibu wa uongozi wa serikali ya mtaa ya eneo hilo, mzazi huyo anatarajiwa kufikishwa kizimbani wakati wowote kuanzia sasa ili kujibu tuhuma za ukatili dhidi ya mtoto baada ya ripoti ya madaktari kutolewa.
Hata hivyo, hii sio mara ya kwanza kwa visa vya ukatili dhidi ya watoto kuripotiwa.

Kumekuwa na matukio mbali mbali yanayogusa nyoyo za wengi huku la hivi karibuni zaidi likiwa ni lile la mtoto Nasra aliyefariki dunia baada ya kuwekwa kwenye boksi kwa muda.
BBC

No comments:

Post a Comment