Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 26 June 2014

NIGERIA KUIVAA UFARANSA, ARGENTINA NA USWISI RAUNDI YA PILI

Valencia alioneshwa kadi nyekundu
Ufaransa ilikamilisha mechi za makundi kwa sare tasa dhidi ya Ecuador.
Licha ya sare hiyo Ufaransa ilisalia kileleni mwa kundi E ikiwa na alama 7 moja zaidi ya Switzerland iliyoisakama Iran katika mechi ya mwisho.
Les Blues walifuzu katika raundi ya 16 bora ambapo sasa watachuana na Nigeria .
Mechi hiyo ilishuhudia kadi nyekundu ya nane katika mashindano haya ya kombe la dunia ,nahodha wa Ecuador Antonio Valencia alipofurushwa uwanjani baada ya kumchezea vibaya Lucas Digne.
Hadi kufikia hapo Ecuador ilikuwa imepoteza nafasi nyingi tu za wazi Valencia na Cristhian Noboa wakiboronga mbele ya lango.
Ufaransa kwa upande wao pia walinyimwa mabao mengi na kipa machachari wa Ecuador Alexander Dominguez aliyelazimika kufanya kazi ya ziada usiku kucha .
Ufaransa itachuana na Nigeria katika mkondo wa pili wa kombe la dunia.
Equador walihitaji ushindi ili kuendelea mbele lakini walishindwa kuvunja ngome ya Les Bleus na hivyo safari yao Brazil ikafikia kikomo hapo.
Ufaransa sasa itakwaruzana na Nigeria waliomaliza mechi yao ya kundi F kwa kushindwa na Argentina kwa mabao 3-2 siku ya Jumatatu tarehe 30 katika Estadio Di Nationale.

Washindi wa kundi hilo Argentina watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Switzerland Jumanne ijayo katika uga wa Arena De Sao Paulo.
Ratiba ya hatua ya mtoano inaonyesha kwamba, Brazil itacheza na Chile; Mexico na Uholanzi; Colombia na Uruguay; na Ugiriki na Costa Rica.
BBCSWAHILI

No comments:

Post a Comment