Nyota: Lionel Messi (juu) aliifungia mabao mawili Argentina dhidi ya Nigeria.
TIMU ya Taifa ya Nigeria maarufu kama Super Eagles imefanikiwa kufuzu hatua ya 16 ya kombe la dunia licha ya kufungwa mabao 3-2 dhidi ya Argentina.
Mshambuliaji hatari wa kikosi cha Alejandro Sabella, Lionel Messi amefunga mabao mawili katika dakika ya 3 na 45 katika ushindi uliowapa Argentina ushindi wa asilimia 100 katika kundi lao la F.
Bao la tatu la Argentina limefungwa na Marcos Rojo katika dakika ya 50.
Mabao mawili ya Nigeria yamefungwa na Ahmed Musa katika dakika ya 4 na 47.
Katika michuano ya mwaka huu, dhahiri, Argentina inamtegemea zaidi Messi katika mechi zake.
Baada ya kufunga mabao hayo, kocha Sabella alimpumzisha nyota huyu wa FC Barcelona kwa ajili ya mikikimikiki ya hatua ya 16.
Pia Sabella alishuhudia mshambuliaji wake, Sergio Kun Aguero akitolewa nje ya uwanja kwa kile kilichoonekana kupata maumivu ya misuli tena.
Mtu muhimu: Messi (kulia) akifunga bao la kuongoza baada ya dakika tatu tu kupita
Asante mungu: Messi akinyosha vidole kama ishara ya kumshukuru mungu baada ya kufunga .
Kusoma zaidi takwimu za mchezo bofya www.bkmtata.blogspot.com
CHANZO FULL SHANGWE
No comments:
Post a Comment