Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 26 June 2014

EXIM FC YAICHAPA PWC 5-2 MECHI YA KIRAFIKI

exim pwc 1Kiungo wa timu ya Exim Bank FC,Mustafa Juma (kulia) akikokota mpira wakati wa mechi ya kirafiki na timu ya PWC iliyochezwa katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Exim Bank FC ilishinda kwa magoli 5 – 2. (Picha na mpiga picha wetu).exim pwc 2Mchezaji wa timu ya Exim Bank FC,Edwin Setebe akikokota mpira wakati wa mechi ya kirafiki na timu ya PWC iliyochezwa katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Exim Bank FC ilishinda kwa magoli 5 – 2. (Picha na mpiga picha wetu).
……………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu,
TIMU ya Benki ya Exim maarufu kama ‘Innovation Team’  imeichapa PWC mabao  5 – 2 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wakati wa mechi hiyo iliyoshuhudiwa na watazamaji mbali mbali, timu ya Exim FC iliyoongoza kwa upande wa umilikaji mpira na kuweza kujipatia goli la kwanza katika dakika ya 20 shukrani zikimwendea mchezaji Lusajo Adam,  wakati katika dakika 22 kiungo Norbert Misana aliipatia timu hiyo goli la pili, mpaka kipindi cha kwanza kinaisha Exim FC ilikuwa ikiongoza kwa goli 2-0.
PWC walifanya mabadiliko katika kipindi cha pili yaliyowaletea matunda na kuweza kupata magoli katika dakika ya  47 na 54 ya mchezo baada ya kupata nafasi mbili za wazi kutokana mabeki wa timu ya Exim FC kushindwa kuwazuia washambuliaji wa PWC kuto funga magoli ya kusawazisha.
Exim FC kupitia mchezaji Norbert Misana aliweza kufunga mabao mengine mawili, goli la tatu likifungwa katika dakika ya 55 na goli la nne likipachikwa kimyani katika dakika ya 70 ya mchezo kabla ya Rogers Timoth kumalizia karamu ya mabao katika dakika ya 85 lililowawezesha Exim FC kuibuka na ushindi baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa.
Akizungumza muda mfupi baada ya kipenga cha mwisho cha mchezo kupulizwa, Norbert Misana ambaye aliibuka mchezaji bora wa mechi hiyo alisema mechi hiyo ilikuwa rahisi zaidi ikilinganishwa na mechi zao nyingine zilizopita.
“Tumecheza mchezo mzuri zaidi ukilinganisha na mpinzani wetu.  Leo timu yetu ilikuwa imejipanga vizuri zaidi hususani katika nafasi ya katikati, na ndiyo maana tuliweza kuudhibiti mchezo kapita vipindi vyote. Tumeweza kucheza kitimu  katika muda wote wa mchezo kitu ambacho kimetusaidia tuweze kutengeneza nafasi nyingi za magoli.
“Wapinzani wetu, PWC ni timu bora, lakini leo nadhani timu yetu, kila mchezaji amekuwa katika fomu kutokana na mazoezi  ya kutosha tuliyokuwanayo na tunaamini tukiendelea na hali hii, timu yetu itafika mbali kimchezo.
“Tumekuwa tukifanya mazoezi kila mwishoni mwa wiki. Hali hii ya mazoezi kwa wiki sio tu inatujenga kiuwezo ili kumfunga kila tunaekutana nae lakini pia yanatuweka imara kiafya na kiakili na hivyo kuweza kutekeleza majukumu yetu vizuri na kwa ufanisi kama wafanyakazi wa Benki ya Exim,” alisema Norbert Misana.

CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment