Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 26 June 2014

NDUGAI ATULIZA MZUKA WA WAFANYABIASHARA KIBAIGWA


 Wiki iliyopita Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai, alifanya ziara katika Kata ya Kibaigwa na kuzungumza na wapigakura wake hao wanaokabiliwa na kero mbalimbali.
Katika ziara hiyo, ambapo alifanya mikutano miwili - mmoja katika Kijiji cha Kinangali na mwingine Mtaa wa Karume, Kibaigwa, Ndugai alizungumzia mambo mbalimbali ya maendeleo, lakini akaonya kwamba siyo vyema wananchi kufanya vurugu kama zilizotokea kwenye mji huo mdogo mwezi uliopita na kusababisha uharibifu wa mali na uvunjifu wa amani.
Vurugu hizo zilitokana na kupandishwa kwa ushuru wamazao ya nafaka, ambapo wafanyabiashara na wakulima waliandamana kupinga kwa maelezo kwamba unazidi kuwabana.
Ndugai alisema ushuru wa mahindi utatozwa sokoni na kwamba ushuru wa karanga umepunguzwa kutoka Shs. 3,000 za sasa hadi 2,000 wakati ambapo ushuru wa mkaa na mazao ya misitu sasa utaachwa kwa maofisa maliasili ili kuondoa kero na usumbufu uliokuwa ukijitokeza.
Kero za maji, umeme na migogoro ya ardhi nayo ilitolewa ufafanuzi na maofisa mbalimbali, wakiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, White Zuberi, Mjumbe wa NEC, Mkanwa, na maofisa wengine alioambatana nao.
Pichani Ndugai akijibu baadhi ya hoja za wananchi waliohudhuria mkutano katika Kijiji cha Kinangali.
 Hapa Ndugai akisalimiana na vijana wa CCM baada ya kumaliza mkutano katika Kijiji cha Kinangali.

Kiu imebana. Mhe. Ndugai akipoza koo wakati akisikiliza maswali kutoka kwa wananchi.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kinangali wakihoji masuala mbalimbali katika mkutano huo.
Eti hapa nijibu nini? Inaelekea ndivyo Ndugai anavyowauliza Mjumbe wa NEC na Katibu wa CCM Wilaya ya Kongwa katika mkutano wa hadhara Kinangali, hasa baada ya kuibuka kwa hoja kwamba ofisi ya chama imemilikishwa kwa mtu binafsi.
Diwani wa Kata ya Kibaigwa, Richard Kapinye 'Kaso' akitoa maelezo kwa wananchi kujibu hoja mbalimbali.
 Akinamama na watoto nao walihudhuria mkutano huo. 
 Naam, hapa Ndugai akizungumza na wakazi wa Kibaigwa katika mkutano wake wa pili uliofanyika kwenye mji huo mdogo.  
 Ngoma ya akinamama ndiyo iliyotanguliza kutumbuiza.
 Naibu Spika hakujivunga, akaamua kuserebuka baada ya vijana wa muziki wa kizazi kipya kuimba kwa ustadi.
 Sehemu ya umati wa mamia ya wakazi wa Kibaigwa wakisikiliza kwa makini.


No comments:

Post a Comment